SAKATA LA AKAUNTI YA ESKROW: MHARIRI EVARIST MWITUMBA UMENISONONESHA!
-- NA Elias Mhegera
Kwanza naomba nikusalimie kwa jina la Bwana muumba wa mbingu na dunia, na kisha nikutakie heri ya mwaka mpya! Siku ya juzi niliona comments zako zikiunga mkono uchambuzi kuhusiana na sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, sikuridhishwa na comments zako na ndiyo maana nimeandika hoja hizi.
Nikirejea katika mada yenyewe kuhusiana na sakata la akaunti hiyo, kwanza naomba nikiri kwamba kwa tabia yangu binafsi huwa sipendi sana malumbano, hususani na wanataaluma wenzangu katika jambo lolote lile.
Pili naomba nikiri kwamba na mimi nimekuwa nikisikia fununu kwamba miongoni mwa sababu za kukuzwa sana kwa sakata hili ni jaribio la 'vigogo' kadhaa kuandaa mazingira ili Prof. Sospeter Muhongo alinyakue jimbo la Wakili, na Mbunge wa Musoma Vijijini Mhe. Nimrod Mkono.
Inadaiwa kwamba Prof. Muhongo analindwa kwa nguvu zote kwa sababu ni mbabe na anaweza kuendelea kuwalinda vigogo waliohusika na ufisadi katika mikataba ya mafuta na gesi asilia, rejea sakata la Muhongo kuwalinda watendaji wa TPDC.
Tutakwenda mbela na kurudi nyuma, lakini jambo moja ni dhahiri, kuna ufisadi mkubwa unaowahusu viongozi wetu wakubwa, ambao sasa tunawataka wajimalize wao wenyewe! Soma dhana hiyo katika novel ya James Hadly Chase: You Find Him-I'll Fix Him, hebu ichote hapa: file:///C:/Users/USER/Desktop/james-hadley-chase-you-find-him.pdf
Novel hii inaelezea jinsi ambavyo muovu anaaminika, na anatakiwa kuchukua hatua juu ya wale wanaoonekana kwamba ni 'waovu'! ni dhahiri kwamba muovu huyo atajitahidi kuwalinda kwa nguvu zote kwani ndani ya nafsi yake anafahamu fika kwamba yeye ndiye kawaponza hao wanaoonekana kwamba ni waovu/wahalifu-hiyo ndiyo Escrow!
kutokana na maslahi mapana ya taifa, na pia mazingira yanayolizunguka sakata hilo mpaka sasa, nalazimika kutoa mchango wangu, tena kwa majonzi makubwa kwa sababu nalazimika kutaja mambo ambayo yatawagusa watu ambao kwangu siyo kwamba ni marafiki wa karibu bali wengine ni ndugu zangu wa damu.
Hata hivyo udugu wetu huo nisingependa unifunge mdomo wangu pale ninapoona kwamba madhara ya mimi kukaa kimya ni makubwa kulikoni kuyaweka wazi niyafahamuyo kwa manufaa na mustakabali wa taifa zima. Nimeisoma makala ya Kazi Msemakweli akiwatetea vilivyo maprofesa wawili, Sospter Muhongo na Anna Tibaijuka.
Kwa vile kauli zifuatazo "Nashawishika kuamini ukweli huu" na "Nimependa uchambuzi huu wa sakata la Escrow, soma hapa" zikihusiana na makala "Sayansi ya hoja na mantiki katika Escrow Account" ni zako (Mwitumba), mimi nakwazika kidogo, na kama nitakuwa nimekukwaza wewe pia kwa mchango wangu basi naomba uniwie radhi.
Nakwazika kwa sababu wewe ni mwandishi mahiri na mhariri mkongwe uliyepata kuongoza gazeti la habari za uchunguzi la This Day, ina maana michezo iliyotumika katika kutengeneza makala ile kwa ngazi yako wewe, uzoefu na uelewa ni sawa na mtoto wa chekechea kumfundisha profesa taaluma yake!
Maneno "NASHAWISHIKA KUAMINI UKWELI HUU???!" badala ya "NASHAWISHIKA KUAMINI MAONI/UCHAMBUZI HUU" kidogo yanakwaza hasa yanapotoka katika fikra pevu za mwana taaluma mkongwe kama wewe. Hivi mpaka sasa bado unaamini kwamba kuna ukweli wowote katika sakata la Tegeta Escrow?
Unazungumzia ukweli upi? Ule unaoetetewa na Rais Kikwete, na timu yake ya akina Prof Muhongo? Eliakim Maswi, Prof Tibaijuka n.k. je ulisoma alichokieleza Prof. Benno Ndulu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania? Je umeyasoma majina ya wahusika wengine waliochota pesa hizo kama walivyoandikwa katika toleo moja la gazeti la Jamhuri?
Kisha nairejea kauli yako nyingine: "Nimependa uchambuzi huu wa sakata la Escrow, soma hapa" hivi hapo kuna uchambuzi kweli ndugu yangu Mwitumba? Mimi binafsi nimeona pumba tupu zilizoandikwa na waandishi 'mamluki' yaani wa kukodiwa 'hack writers' au 'mercenary journalists' watu ambao hulipwa pesa na kuandika upumbavu wowote wanaoelekezwa na mlipaji wao.
Nilitegemea kwamba kwa kuwa wewe umekaa kwenye chumba cha habari kwa muda mrefu kuliko mimi ambaye kwa muda mwingi nimekuwa nikiandika kama mwandishi wa kujitegemea na nimekaa katika chumba cha habari kwa muda usiozidi miaka sita (6) mpaka sasa, ungekuwa na upeo mkubwa zaidi wa kuunganisha mambo kulikoni mimi.
Kisha nataka nirejee katika jina la mwandishi mwenyewe anayeitwa KAZI MSEMAKWELI, binafsi katika taaluma yangu ya utambuzi wa majina niliyoipata wakati nikiwa Afisa Uhamiaji, hata jina lenyewe tu lina utata na linaacha maswali mengi kuliko majibu!. Mwandishi huyo ukiangalia jinsi alivyojenga hoja kwa hali yoyote ile ni mwandishi mkongwe.
Lakini ukienda kwenye facebook mtafute kwa jina hilo hapatikani, nenda tumia google search hapatikani, basi tafuta hata picha yake tu, haipatikani!. Ni dhahiri huyo ni mwandishi 'ruhani' ni mwandishi wa kutunga 'fictitious' au ni mwandishi jinni kitaaluma anakaribiana mno na hao 'ghost writers' ambao kazi yao ni kuandika fikra za watu wengine na wala siyo fikra zao wenyewe.
Ukiachana na jina lake nenda hata katika gazeti au magazeti ilipotumika makala hiyo, nimeisoma makala hiyo nzima yenye kurasa tatu na imeelezwa kwamba ilitumika kwa mara ya kwanza katika gazeti la Alhuda na ndipo ikahamishiwa katika gazeti la Taifa Imara.
Kimsingi magazeti haya yote mawili yamo katika mfumo wa umiliki unaoitwa 'Quasi-independent' kwa maana ya kwamba si magazeti huru bali ni magazeti huru nusu nusu! Kabla ya makala hii, gazeti la Taifa Imara liliwahi pia kuandika kwa "Wakatoliki wakerwa kwa maaskofu wao kudhaliishwa" uandishi wa ain hii mimi naona kwamba ni upuuzi mtu!
Ukitaka kuyafahamu kwa vile wewe ni mtaalamu basi fanya utafiti mdogo wa 'content analysis' rejea magazeti ya aina hii yaliandika nini kwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010! Kwa mfano An Nuur, Tazama Tanzania, Sauti ya Umma, na hata Changamoto yalijikita katika kuandika kwamba Dkt Slaa katumwa na Kanisa katoliki, kapora mke wa mtu, na hata kuunga mkono pale Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lilipotoa vitisho.
Magazeti mengine yaliyounga mkono habari hizo vikiwamo vitisho vya JWTZ ni Daily News, Uhuru, Jambo Leo, Habari Leo, An-Nuur etc. uwiano wa sera kati ya magazeti haya na yale ya serikali na chama cha Mapinduzi ni kiashiria tosha kwamba hayo siyo magazeti huru bali yanafadhiriwa na watawala wetu wa sasa.
Natoa mifano michache: Tazama Tanzania Na.417, Oktoba 30, 2010 "Sababu za kutomchagua Dk Slaa kesho hizi hapa" Tazama Tanzania Na. 419, Nov 9-15, 2010 "kwa nini Kanisa Katoliki linataka kutupokonya Nyerere wetu?" An-Nuur 912, Septemba 28, 2010 "Tuhuma za uporaji wake za watu zitazamwe," na katika toleo hilo hilo: "Kikwete kawakosea nini maaskofu"
Ann Nur, Toleo Na. 903, Septemba 17-20, 2010 "CHADEMA ya walokole, akina Zitto mamluki?" Pia katika toleo hilo hilo "Slaa ni chaguo la Katoliki" An Nuur Na. 903, Agosti 20-26, 2010 "Padri anaweza kuwa mtawala bora"
Mifano ipo mingi naomba nisiende zaidi katika hilo. Kuhusu gazeti la Taifa Imara ambalo mimi naamini bado ni jipya, ni miongoni mwa magazeti hayo hayo niliyoyazungumzia ambayo ni nusu huru, na yanalipwa na watawala wetu na kwa hiyo habari zake haziwezi kuaminiwa na watu makini aina ya Bw. Evarist Mwitumba.
Kuhusu migao ya pesa za Tegeta Escrow, kila mfuatiliaji makini atagundua kwamba huu ni muendelezo wa sakata la EPA, kwa sababu baadhi ya wanufaika wa pesa za EPA sasa tena ni wanufaika wa hizo za Escrow! Nani asiyefahamu kwamba Jaji Mujulizi alitokea katika kampuni ya mawakili ya IMMMA Advocates ambao walinufaika na pesa za EPA, mazingira ya uteuzi yake ni yapi, ni kwanini tena jaji huyu yumo kwenye mgao wa Escrow?
Kama pesa hizo ni halali mbona aina ya mgao uliofanyika unafuata mkondo yote ya fedha chafu zilizotakatishwa? Mbona Askofu Kilaini ni kiongozi pekee wa Kanisa Katoliki aliyepata kusema kuwa 'Bw. Mafuta Mengi' kwa kuazima msemo wa Wakenya ni chaguo la Mungu na sasa anapata mgao wa Escrow?
Ni nani asiyefahamu ubia wa Prof. Tibaijuka a.k.a jembe na 'Bw Mafuta Mengi' katika uporaji mkubwa wa ardhi? Mfano halisi ni jinsi alivyolazimisha kugawa ardhi kwa kampuni ya "mwekezaji bandia" ya Eco-Energy katika maeneo ya Bagamoyo?
Kwa mfano mimi nilipofuatilia katika Idara ya Uhamiaji makao makuu afisa wa vibali vya makazi akaniletea mafaili matano ambapo mwekezaji huyo amechukua ardhi kubwa, ambayo hata hivyo haifanyiwi kazi yoyote zaidi ya kuwapora wakulima wanyonge.
Nilipomhoji je ni kwa nini mwekezaji huyo anaishi Tanzania kuanzia mwaka 2007 mpaka mwaka huo (2014) bila kazi yoyote ki-Uhamiaji tunamuita ni mkazi mzigo (destitute) na serikali haijachukua hatua yoyote?
Afisa huyo wa uhamiaji akanijibu "Bw. Elias, ndugu yangu, naomba achana na jambo hili, Tanzania ya leo siyo ya jana, unaweza kustukia mtu anakuchoma kisu chenye sumu kali mgongoni mwako na ukapoteza maisha yako, na muuaji asipatikane!, tulia tulee watoto ndugu yangu!" mwisho wa kumnukuu.
Kwa tafsiri yangu mwekezaji wa Eco-Energy ni muajiriwa wa Mtanzania tajiri na mwenye mamlaka (kama ilivyokuwa kwa IPTL, rejea kauli ya Mhe. Tundu Lissu kabla hajingiliwa na 'Dr' Mary Nagu, na ndiyo maana anaweza kuishi nchini bila usumbufu na adha zozote toka Idara ya Uhamiaji.
Binafsi nimefanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Eco-Energy Bw. Anders Bergfors ofisini kwake na pia Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Ahmed Kipozi na wote walijikanyaga tu katika majibu yao. Kwa hiyo Prof Tibaijuka alikuwa analipwa ujira wake kwa kufanikisha uporaji mkubwa wa ardhi haijalishi pesa hizo zilipitia miononi mwa nani iwe Rugemalira au Ruge-maliza!
Askofu Kilaini vivyo hivyo alikuwa anapata mgao wa shukrani kwa kusimama hadharani na kumfanyia mwanasiasa kampeni kinyume na msimamo wa kanisa lake. Viongozi wengine kama Askofu Nzigilwa na mapadri wanaweza kuwa wametumika tu ili kuficha lengo hatuwezi jua labda wanaandaliwa kwa ajili ya kusaidia kampeni za 2015.
Prof. Muhongo anafahamika kwa ubabe wake wa kukataa kutoa mikataba katika sekta ya mafuta na gesi asilia kama sheria na mikataba ya kimataifa inavyotakiwa yaani kuwa ya wazi badala kuwa mali na siri ya serikali pekee.
Rejea vipengele hivyo katika African Peer Review Mechanism (APRM) na Open Government Partneship (OGP) inavyoagiza. Kuhusu utakatishaji wa fedha ni somo ninalolifahamu kwa kina.
Nilipata mafunzo juu ya utakatishaji wa pesa kutoka taasisi ya kupambana na utoroshaji wa watoto, yaani African Network for The Prevention & Protection against Child Abuse and Neglect (ANPPCAN) na mpango wa kupambana na ufadhili kwa ugaidi na uhalifu mwingine mkubwa.
Pia nimewahi kupata mafunzo mengine kama hayo kutoka kwa taasisi ya Financial Transparency Coalition, chini ya asasi ya Policy Forum.
Hivyo basi kilichofanyika katika benki za Mkombozi na Stanbic ndiyo hicho hicho hufanyika katika utakatishaji wa pesa chafu za kiharamia je ni kwa nini iwe hivyo? Yaani akaunti inafunguliwa, pesa zinawekwa na kuchotwa kisha akaunti inafungwa! Bado kuna utetezi hapo jamani? Je kweli hiyo ni pesa safi? Kwa nini iondolewe katika njia chafu? Njia za hofu hofu?
Unaweza kusoma kitabu cha Paul Allan Schott: Reference Guide to Anti-Money Laundering and Combating the Financing of Terrorism, kwa uelewa zaidi kipate hapa: http://siteresources.worldbank.org/…/Reference_Guide_AMLCFT…
Hitimisho
Naamini wasomaji watapata mwanga ni kwa nini maprofesa hao 'majembe' wamekuwa na viburi na kujiamini sana ni kwa sababu wanajiona kwamba wao wazijua siri za 'wakubwa' kwa undani zaidi, yaani Muhongo katika suala la mikataba ya mafuta na gesi asilia na Tibaijuka kuhusu uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali za nchii (rejea lugha ya tulimuita, tukazungumza tukamuomba…)
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU UBARIKI TANZANIA

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments