Habari watanzania wenzangu wapenda amani na maendeleo.Napenda kuchukua nafasi hii kutolea ufafanuzi suala la nani ni mmiliki wa Naf Beach Hotel iliyopo mkoani Mtwara.Kumekuwa na habari zikisambaa kwa muda mrefu sasa juu ya kuhusishwa kwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika umiliki wa hoteli hii ya nyota tano.
Ukweli ni kwamba Membe hajawahi kumiliki au kuwa sehemu ya umiliki wa hoteli hii.Membe hajawahi kufanya biashara.Kumhusisha Membe na umiliki wa Naf Beach Hotel ni kuchuma dhambi kwa muumba wa vyote duniani.Tusitumie siasa chafu kuchafua hata wasiohusika na mambo yanayozushwa mitaani.Hoteli ya Naf Beach ni mali ya Shabaan maarufu kama Shebby Mix aliyoijenga kwa mkopo kutoka Crdb.
Hakuna uhusiano wowote kati ya Membe na Shabaan iwe kiundugu,kiurafiki au kibiashara na ndio maana inakuwa sio afya kuleta mijadala inayosema uongo kuhusu hoteli hii isiyokuwa na jina lenye nasaba yoyote na Membe katika umiliki wake.Nasisitiza tujadili kweli na kuikataa uongo kwasababu itatuweka huru kifikra na kimaamuzi.Nawasilisha!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments