[wanabidii] MAASKOFU TISA AICT WATEMBELEA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO

Friday, January 16, 2015
MAASKOFU TISA AICT WATEMBELEA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO
Na Happiness Katabazi
KANISA la Africa Inland Church Tanzania (AICT) imenifanya ibada Maalum Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB) na Kusema Kuwa uanzishwaji wa chuo hicho uliofanywa na Wahadhiri wastaafu ni mpango wa Mungu.

Hayo yalisemwa Jana mchana na Kiongozi wa Msafara wa Jumla ya Maaskofu tisa wa Kanisa hilo la AICT , Askofu Dk.John Nkola toka Dayosisi ya Shinyanga alisema wamefika katika Makao Makuu wa UB ,Mikocheni Dar es Salaam, alisema wakati Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Profesa Costa Mahalu na wenzake walipokuwa ma wazo la kuanzisha UB ,walimkabidhi Mungu wazo hilo na kwamba viongozi wa dini mara kwa mara waliyoiweka wazo Hilo kwenye maombi na hatimaye UB ilianzishwa rasmi mwaka 2011 na waanzilishi wa UB ni waliokuwa waadhiri wa Vyuo Vikuu Vya Serikali ambao walistaafu kazi Katika Vyuo Vikuu Vya Serikali na kuamua kuanzisha Chuo Kikuu chao cha UB.

' Tumekuwa tukiisikia UB ,leo tumefurahi kufika na kuiona na zawadi tunayoitoa kwa UB ni kuwafanyia maombi kwa Mungu ili UB izidi kupiga hatua kimaendeleo katika sekta ya elimu kwasababu hata Maandiko ya Vitabu vitakatifu vinawataka binadamu wakamate sana elimu' alisema Askofu Dk.Nkola.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu UB, Profesa Costa Mahalu aliwashukuru maaskofu wa Kanisa Hilo la AICT ambao wametokea kwenye Dayosisi ya Mwanza, Geita,Mara-Ukerewe, Shinyanga,Tabora na Pwani kutembea Makao makuu ya UB - Mikocheni B , na kufanyia Maombi chuo hicho na kupata maelezo mbalimbali na kwamba maskofu hapo ambao wametokea Mikoa tofauti na wamekuja Dar es Salaam kwaajili ya Kuja kushiriki kwenye Sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la UB Katika Kijiji cha Kiromo wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani itakayofanyika Januari 17 Mwaka huu ,ikiwa ni Ishara ya Kuanza kwa Ujenzi wa Makao makuu ya UB Katika Kijiji cha Kiromo.

Chanzo: Facebook: Happiness Katabazi
Januari 16 Mwaka 2015.


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments