[wanabidii] KUVULIWA UANACHAMA AU KUKATWA JINA LA LOWASSA

Monday, January 12, 2015

KUVULIWA UANACHAMA AU KUKATWA JINA LA LOWASSA

Kama jambo hilo kweli ni moja ya Agenda zilizopelekwa mezani, Mimi naamini INTELLECTUALS hawa wanaounda KAMATI KUU ya CCM hawataruhusu majungu na fitina ziwatawale. Na kwanini iwe Lowassa wakati matano kwa makumi ya wanasiasa wanaonekana wazi katika heka heka mbali mbali? Wengine wakiwa wameshatekeleza haki yao ya kikatiba na kikanuni Ibara ya 32 Kifungu na. 1 ya kutangaza nia wakati wowote kama kanuni hiyo inavyosema. Wengine wametangaza nia wazi wazi na wengine wametangaza nia kimya kimya ingawa ilisikika. Naamini KAMATI KUU inatambua fika kuwa maamuzi yao yaliyopita ambayo mimi naamini msingi wake ulikuwa ni majungu, yaliwakosesha matumaini masikini na wahitaji wengi ambao Lowassa alikuwa kimbilio lao kubwa katika kuongoza Harambee zao, ambazo kwa hakika kutokana na nuru ya Lowassa, nuru inayowaumiza baadhi ya watu, zilikuwa ni zenye mafanikio makubwa. Maelfu ya Vijana wa Boda Boda walikosa matumaini baada ya matarajio yao ya Harambee kubwa kupata kutokea kuzimika ghafla. Makundi mengi ya kijamii yaliyopeleka maombi kwa Lowassa yalipoteza matumaini ya kupata ufumbuzi wa haraka wa matatizo yao. Nakumbuka hamasa kubwa waliyopata wananchi wa kwaida, wazazi na watu mbali mbali wa Mbagala, walijitokeza kwa maelfu pale St. Anthony waliposikia Mhe. Edward Lowassa ndio Mgeni rasmi, na hatimaye kila mtu akiwa na furaha walichangia kwa nguvu kubwa mpango wa madawati na mambo mengine kwa shule za Mbagala. Siku hiyo kwa hamasa ya Lowassa mwenye elfu 5 alitoa, Mwenye elfu 10 alitoa, mwenye laki alitoa, mwenye elfu 50 alitoa, mwenye laki tano alitoa, mwenye Milioni alitoa hatimaye milioni 220 zilipatikana na matatizo mengi yakarekebishwa kwenye shule za Mbagala. Ingawa wabaya wa Lowassa na wafata mkumbo wakatangaza Lowassa amemwaga milioni 220 kwenye shule za Mbagala. Katika hili linalozungumzwa maamuzi yatokanayo na msukumo wa uzushi na mambo ya kutungwa yanaweza kuweka historia mbaya kwa Chama Cha Mapinduzi. Rai yangu kwa KAMATI KUU watambue kuwa Lowassa ana maadui wakubwa wanaendesha vita kali ya kisiasa, maadui hao wamepandikiza watu katika maeneo mbali mbali. Sasa taarifa wanazoletewa kuhusu Lowassa wasikimbilie kuziamini kwani Majungu, fitina na mambo ya kutungwa yamewekwa Mbele sana katika kukabiliana na Lowassa.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
MUNGU IBARIKI TANZANIA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments