KANISA KATOLIKI TUAMBIENI KILICHOMUONDOLEA WITO WILBROAD SLAA
Ndugu wapendwa nawasalimu kwa jina la yeye aliyejuu.
Wakati tukielekea kuwapata viongozi wa kitaifa hapo mwezi Oktoba mwaka huu wa 2015, nimeona leo niliombe Kanisa Katoliki lituaidie kutegua hiki kitendawili hiki cha muda mrefu cha mmoja wa watajwa wenye nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao alikuwa akilitumikia katika nafasi za juu kabisa za uongozi.
Naamini Kanisa linajua vema sababu za WILBROD SLAA kuacha kuitumikia Kanisa kama Padre. JE alifukuzwa au aliacha mwenyewe na kwa sababu gani? Tupate kujua ili kipindi hiki ambacho tunaelekea kuwa naye kwenye harakati za kuusaka urais tupate kujua tuna mgombea wa aina gani.
Mimi ni mzaliwa wa Mkoa wa Arusha na mwenyeji wa mji mdogo wa Manyara, njiani kuelekea nyumbani kwa Wilbroad Slaa yaani KARATU.
Nimeishi kwenye mkoa wangu tangu nimezaliwa, nikasomea elimu yangu ya msingi hadi sekondari kabla ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kwa sasa naishi Dar kutokana na mihangaiko ya hapa na pale ili mkono upate kwenda kinywani
Kanisa Katoliki mara kadhaa limekuwa likikumbwa na kashafa za aina mbili na hasa mkoa wa Manyara na Arusha hususan majimbo ya Mbulu na Karatu, Kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za Kanisa na ile ya Mapadre kujihusisha na Mapenzi kinyume na Sheria za Kanisa, nitatoa mfano.
PADRE mmoja wa jimbo la Mbulu(jina nalihifadhi ila kama kuna mwingine anaifahamu hii scandal anaweza kumtaja ili kudhihirisha ukweli wa mfano huu) aliwahi kuchukua fedha za kanisa mil.300 akazipeleka kwa mganga wa kienyeji ili zifanyiwe madawa kwa kuamini kuwa zitaongezeka, kilichotokea ni mganga yule kutokomea na zile pesa bila Padre kujua . Sakata hili liliwagharimu sana waumini kwani walilazimika kutoa sadaka 3 badala ya 2 kama ilivyo kawaida ili kufidia pesa zilizopotea. Nakumbuka Sakata hilo lilimhusisha pia Makamu wa Askofu jimbo la Mbulu wakati huo akiwa father John Nada ambapo Askofu wa jimbo hilo akiwa Yuda Thadei Rwaichi ambaye hivi sasa ni askofu wa jimbo la Mwanza.
Kuhusu kashfa ya Mapenzi, namfahamu PADRE mmoja (jina nalihifadhi) ambaye hivi sasa kituo chake cha kazi kipo KARATU, huyu ameoa na ana watoto, Mke wake alikuwa mwalimu wa shule moja ya sekondari ya kata pale Mbulu mjini ambaye kwa sasa yuko ofisi ya utamaduni katika halmashauri ya Wilaya Mbulu.
Nirudi sasa kwenye hoja msingi, pamoja na mifano hiyo miwili bado Kanisa limeendelea kuwavumilia watu hao na mpaka leo ni watumishi wazuri tu wa Mungu, Swali langu ni kosa gani kubwa ambalo SLAA alifanya ndani ya kanisa? NI muhimu sana tukaambiwa
ZIPO TETESI kuwa mambo yaliomuondoa SLAA kama mtumishi wa Mungu aidha kwa kufukuzwa ama yeye mwenyewe kuona aibu kuwa ni pamoja na:
Kuhujumu mradi wa ujenzi wa Nyumba za Masista kule Kurasini jijini Dar es Salaam wakati akiwa Katibu wa Maaskofu.
Kuweka kibindoni pesa nyingi zilizopatikana kutokana na maandalizi ya ujio nchini wa papa John Paul wa pili wakati yeye SLAA akiwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.
Kanisa tuambieni SLAA alifanya nini huko?
Mbali na hayo ambayo Kanisa lingetusaidia kumhusu Wilbroad Slaa, lakini pia ingependeza kama SLAA yeye kama yeye pamoja na kuyajibu hayo ambayo tunawasumbua viongozi wake wa kiroho pia atujibu haya yanayoongelewa mtaani kuwa:
Kupitia Hospitali ya CCBRT alitengeneza mradi hewa wa kujenga hospitali ya kisasa kabisa eneo la mlalakua jijini Dar es Salaam ili apate msaada kutoka kwa wafadhili. Zipo taarifa kuwa kutokana na mpango huo wafadhili pamoja na kukubali kufadhili ujenzi wa hospitali hiyo lakini pia walishampa kiasi fulani cha Magari ambayo yaliingizwa nchini pasi kulipa kodi na hayajulikani yalipo.
Nawasilisha.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments