> Makabwela.
> '. (Dkt.Muhammed Seif Khatib )
>
> Kabwele ni mtu wa hali ya chini kiuchumi ambaye hana kipato cha maana.Zaidi hayo
> huweza kuwa mtu ambaye hakusoma na kuonekana mjinga mbele ya jamii.Katika nchi
> yenye matabaka makabwela ndiyo wengi ukiwalinganisha na kundi la wachache wenye
> kumiliki mali, vyeo na ulua.Wachache hawa ndio washikao hatamu za utawala, njia kuu
> za uchumi na vyombo vya ukandamizaji zikiwemo magereza,polisi na mahakama.Ni hao
> hao hudhibiti vyombo vya itikadi kama redio,televisheni,magazeti na makanisa,misikiti
> na mahekalu.Hawa wachache hujiwekea mfumo na utaratibu wa kuzimiliki fursa zote
> ziliomo katika jamii zikiwemo elimu,afya na makaazi.Kikundi hiki kidogo katika jamii
> hujiweka kinasaba,kiukoo na kikabila.Lakini utajiri wao hutegemea nguvu na jasho la
> kundi kubwa la makabwela.
> Kesho Zanzibar inatimiza miaka hamsini na moja tokea makabwela wa Zanzibar
> walipozikata silasila za kutawaliwa na ukoo wa Sultan wa El Busaidy kutoka Oman.
> Seyyid Said bin Sultan aliikita utawala wake Zanzibar mwaka 1832.Zanzibar ikawa
> mali yake pamoja na wakeze, watoto zake na kila aliye wake.Na wale Waswahili
> aliyowakuta wakawe raia wake yeye mtu mmoja.Mwingereza naye akafika Zanzibar
> na kuzamisha mrija wake kuinyonya Zanzibar.Ilikuwa tarehe 14 June mwaka 1890
> pale Mwingereza kuichukuwa Zanzibar na kuifanya Himaya yake.Kazi kubwa ni
> kumlinda Sultan na Usultani wake dhidi ya 'maadui wa ndani na wa nje'.Maadui wa ni
> makabwela na wa nje ni dola za ulaya.Mapinduzi ya makabwela ya tarehe kama ya kesho
> lya Jumapili ya mwaka 1964, kama si kumtoa kwa nguvu Sultan Jamshed kutoka ukoo
> wa Seyyid Said, Usltani ulimiza miaka 132. Miaka yote ya utawala wa ukoo mmoja si
> muda mdogo.Na kama si Mapinduzi, Usltani huo leo ungetimiza miaka 183.Lakini
> makabwela hawa wa Zanzibar waliitawaliwa kwa ubia na Mwingereza.Hata yeye
> wakati anaondoka terehe 10.12.1963 na kujidai kuipa 'Uhuru' Zanzibar ilikuwa tayari
> ameitawala Zanzibar na kuinyonya kwa miaka 73. Miaka hiyo si kidogo.
> Watawala wa Zanzibar kwa miaka yote hiyo walikuwa Waingereza na Sultan
> wa Kiarabu.Hawa ndio waliokuwa wakibwia ziada ya uchumi wa Zanzibar.Waliishi na
> kutunzwa na hazina ya serekali.Sultan wakitawala kwa zamu na watoto wao
> wakisubiri kurithi usultani na hazina ya nchi.Wao watawala, watoto wao,ami zao,shangazi
> zao na shemegi zao wakiishi kugemea utajiri uliotengenezwa na nguvu za makabwela.
> Kama vile hayo hayatoshi mashamba yenye ardhi yenye rutuba wakapora jamaa zao
> mabeanyenye wa Kiarabu.Walimaji,wapandaje na wavunaji ni makabwela.Mapato ya
> ghila na mavuno yote yakiangamia katika matumbo ya Waarabu wachache.Zao la karafuu na mbata liliwapa utajiri usiomithilika wenye mashamba haya huku wale makabwela
> walimao wakifukarika.
> Eneo jengine la utajiri kwa baadhi ya wafanya biashara wa Kiarabu ni utumwa na
> biashara ya utumwa.Waafrika kwa maelefu wanaume,wanawake,watoto na vijana
> waliswagwa kama n'gombe wa machungani walipelekwa Zanzibar mtaa wa Mkunazini
> na kunadiwa sokoni hapo.Wapo waliopelekwa ughaibuni na kuselea huko katika mashamba
> ya miwa,tumbaku na pamba.Wengine wakabakishwa Zanzibar na kifanyakazi katika
> mashamba ya minazi na mikarafuu na wengine kugeuzwa watwana na kufanya kazi za
> majumbani.Watumwa wanawake wakabatizwa kwa kuitwa 'wajakazi' hawa wakawa
> mayaya,wapishi,wakandaji na wanaume na kugeuzwa starehe za kingono kwa
> Sultan na Warabu wenzake.
> Tabaka jengine lilofaidika wakati wa utawala wa Sultan na Waingereza ni la
> wafanyabiashara wa Kihindi.Hawa walifungua maduka ya kuuza bidhaa kutoka nje.
> Walifungua maduka ya rahani na poni.Walikopesha fedha kwa wafanyabiashara wa
> Kiarabu waendao bara na mrima kununua pembe za ndovu lakini wabebaji ni makabwela.
> Mauzo ya mbata na karafuu yakifanywa na Wahindi.Wachukuzi na makuli wa bandarini walikuwa makabwela wa Kiswahili.Bandari ya Zanzibar ik iendeshwa na Wahindi kwa
> kukodishwa na Sutan.
>
>
>
>
> Fursa za elimu bora, matibabu na huduma za maji safi na salama zikitolewa kwa
> tabaka tawala na Waarabu na Wahindi.Kulikuwepo skuli za makabila na dini ambazo
> ziliwatenga makabwela wa Kiswahili.Hata maeneo ya ,kuishi yalifanywa kwa u
> Ubaguzi.Maeneo ya Mji Mkongwe una majengo ya ghorofa yaliyoezekwa kwa bati,
> yenye njia za lami,umeme ndani ya majumba na nje ya majumba.Ndani ya majumba
> hayo yamo maji safi na salama.Wanaoishi huko Sultani na aila yake.Balozi wa
> Kingereza na mabalozi wengine.Maofisa wa serekali wakiwemo mahakimu, wakuu
> magereza na polisi wengi wao wakiwa Waingereza.Mabwanyenye wa Kiarabu na
> mabepari wa Kihindi ndiyo yao maskani yao.Huko hakuruhusiwi kuishi makabwela
> wa Kiswahili. Jua likitua lazima waondoke warudi eneo lao la N'gambo upande
> wa pili wa mji. Huko N'gambo ni mitaa ya mchafukoge. Nyumba za makuti,mbavu za
> mbwa na matope.Hakuna maji zaidi ya mito na visima - yote siyo safi na salama.Hakuna
> skuli hapana hospital.Hakuna barabara zaidi vichochoro vya vumbi,matope na mchanga.
> Nyumba wakaazo makabwela viwanja si vyao.Kila mwezi au mwaka lazima walipe
> Kwa Wahindi wenye viwanja.Makabwela ndio wahadumu wa uchukuzi wa mizigo na
> huko Mji Mkongwe kukicha!Makabwela ndiyo maboi,matopasi,madobi na wachuuzi kwa Mji Mkongwe kila asubuhi.Makabwela wanawake ndiyo wajakazi wanaopika, kuleya watoto
> na wanaosinga wanaume.
> Shamba ndiko kwenye kundi kubwa la makabwela wakweya minazi na wachumaji karafuu.
> Pia ni walimaji na wavuvi.Maisha yao haya kupishana sana na ya makabwela wa N'gambo.
> Hawana umeme wala maji.Hawana hospital wala skuli.Hakuna barabara ya lamPHawa ndiyo walishayo Zanzibar na walimao mazao ya biashara yanayowatajirisha
> aWahindi na Waarabu chini ya ulinzi wa Mwingereza.
> Makabwela walichoshwa na mateso,sulubu na manyanyaso.Udhalilishwaji kwa wanawake kuitwa 'wajakazi' na wanaume kuitwa 'watwana' ulivunja utu na ubinadamu.
> Tabia ya Sutan hawa kuhalalisha zinaa kwa kulala na wajakazi kwa kuwaita
> 'masuria' kuliwaibisha wanawake wa Kiswahili. Makabwela kunyimwa fursa
> za elimu na huduma za kijamii kuliwapa unyonge.Utawala wa Ukoo mmoja tu wa
> Kisultani uliodumu kwa kurithishana na wenyeji kuwa rai wa mtu mmoja kilitosha
> kuumua hasira dhidi ya utawala wa Kisultani.
> Kuundwa kwa chama cha makabwela cha Waswahili Februari tarehe 5 mwaka
> 1957 kulichochea na kuamsha ari ya kuikata minyororo ya kutawaliwa.Kikundi cha
> vijana kumi na nne cha makabwela wakaamua kujitosa katika mkondo wa hatari
> wa kugharikisha maisha yao au kuikomboa nchi na vizazi vinavyofata.Makabwela hawa
> wakaamua waipinduwe serekali ya mseto ya vyama vya ZNP na ZPPP.Wakiongozwa
> na ari,uzalendo na ushujaa waliwaongoza wenzao kuingia katika maboma ya polisi Ziwani na kule Mtoni katika kuikosi cha Police Mobile Force( P.M.F).Ilikuwa siku ya
> Jumamosi tarehe 11 Januari saa nane usiku. Kwa kutumia Silaha za asili za mikuki,
> mishare,mapanga,visu na mawe walifanikiwa kuzishika kambi zote na silaha za moto.
> Mashujaa hawa makabwela wasiokuwa na elimu, wenye kipato cha chini katika jamii na
> wanaonekana wajinga ndiyo walioandika ukurasa wa historia iliyotukuka.Kati yao
> ni wawili tu ndiyo waliobaki hai, wenzao kumi na mbili wameshafariki.Mashujaa hawa ni
> makabwela kweli? Tuone amali na kazi ni zipi ? Miongoni mwao ni John Okello( mvunja mawe na mpaka rangi nyumba)
> Said Natepe(mpaka rangi nyumba),Khamis Darweshi ( kuli),Mohamed Kaujore( mchuuzi
> wa samaki),Said Bavuai (dereva),Yusuf Himid (Dereva P.W.D), Ramadhani Faki, Muhamed
> Mfaranyaki na Khamis Hemed (askari polisi) Seif Bakari (fundi Cherehani) Pili Knamis,
> Hafidh Suleiman na Hamid Ameir (wakulima huko Donge).
> Hawa ndiyo mashujaa wa kweli waliorejesha heshima ya mtu mwesi katika kisiwa
> cha Zanzibar.Kiasi gani wanakumbukwa na kuheshimiwa
>
>
>
>
>
>
> P
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> P
>
>
>
>
>
>
>
>
> ,
>
> Pp
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> Ik
>
>
>
> I
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments