Ndugu zangu,
Ninapomsikiliza Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye kwenye taarifa yake inayotokana na kikao cha Kamati Kuu, Kisiwandui, naipata tafsiri moja kuu; kuwa CCM imebaini, kuwa ' Bahari Ya Kisiasa Imechafuka'.
Wimbi la Escrow ni kubwa mno kwa CCM kulidhibiti kuelekea Uchaguzi Mkuu. CCM inataka kulikwepa. Inataka kwenda kwenye uchaguzi ikiwa na sahani safi na kavu- Not only a clean slate, but a dry one.
Hivyo, CCM haina namna yeyote, bali kuwaacha wote wenye kuhusishwa na Escrow waogelee wenyewe bila kutegemea maboya ya chama. Katika hili, na kwa kupitia taarifa ile ya Nape Nnauye, Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo ametoswa rasmi.
Yawezekana kabisa kuwa Sospeter Muhongo amefanya kazi njema kwa taifa kupitia Wizara yake, lakini, maisha ya kisiasa ni magumu. Hapa hesabu za kisiasa zinamtaka aondoke, kwa kujiuzuru mwenyewe, au kusubiri kuwekwa kando na aliyemteua. Na maisha ya kisiasa yataendelea. Muhongo anaweza kurudi tena kwa nguvu zake mwenyewe.
Maggid ,
Dar es Salaam.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7a3W2XY%2BUtApGBsByesXqmcoY-aN576-r8wiyqYBcCuw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments