[Mabadiliko] " Ewe, Simbachawene, E Nenda Nishati Na Madini Ukasimamie Maslahi Ya Wengi"

Sunday, January 25, 2015


Ndugu zangu,

Nimeupokea kwa matumaini uteuzi wa Rais kwa George Simbachawene kuwa Waziri wetu wa Nishati na Madini.

Nimemsikiliza mara kadhaa George Simbachawene akijenga hoja ndani ya Bunge. Binafsi, kwa kupima hoja zake, naamini kuwa Simbachawene amesimamia upande wa wengi. Simbachawene, Mbunge wa Kibakwe na aliyepata kuwa Naibu Waziri Nishati Na Madini , sio tu anaijua sekta hiyo, lakini, anajua vema jinsi wananchi wa vijijini , kule Kibakwe na kwengineko Tanzania wanavyosubiri kwa hamu wafikishiwe umeme wa gharama nafuu, kazi ambayo, aliyemtangulia Simbachawene, Profesa Muhongo alikuwa akiendelea kuifanya kwa ufanisi.

Simbachawene anatambua, kuwa mwelekeo wetu kama nchi kwa sasa ni wa kiuchumi zaidi. Na kimsingi ni mwelekeo wa dunia nzima. Na kwenye uchumi mkubwa ambao unaweza kuitoa nchi haraka kutoka mahali ilipo na kupiga hatua za haraka za kimaendeleo ni kwenye sekta ya nishati, inahusu madini ikiwamo gesi na mafuta.

Na nchi yetu inaingia sasa kwenye uchumi wa gesi. Inahitajika sana duniani. Hivyo, ghafla, wakubwa duniani wanatuzonga kwa namna nyingi kutaka kunufaika na rasilimali tulizo nazo.

Na pengine ifahamike, kwa wakubwa hawa duniani. Wizara nyeti wanayoiangalia kwa karibu katika nchi yetu ni ya Nishati Na Madini. Hivyo, Waziri mwenye dhamana kwenye Nishati na Madini, kwa wakubwa wa dunia, yumkini ni Waziri Muhimu sana kuliko wengine wote.

Nina mfano, jioni moja, nikiwa Dar es Salaam, nilipata kualikwa kwenye hafla fupi nyumbani kwa Balozi wa nchi moja ya Kimagharibi. Mahala pale kulikuwa na watu wengi, akiwemo tajiri Sir Andy Chande, alikuwepo pia Profesa Baregu. Na mwalikwa mwingine alikuwa Profesa Muhongo. Ajabu ya jioni ile, mtu pekee aliyetambulishwa na mwenyeji wetu juu ya uwepo wake ni Profesa Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania. Jambo hilo linapigia mstari nilichokieleza hapo juu.

Hivyo, tukifanya makosa tukamweka Nishati na Madini, Waziri au watendaji wenye uchu wa mali na madaraka, basi, ni rahisi kwao kutuharakishia laana ya rasilimali. Maana, ni rahisi wakageuka kuwa mawakala wa matajiri wachache badala ya watumishi wenye kusimamia maslahi ya umma.

Na hakika, Nishati na Madini ni kama eneo lililofukiwa mabomu ya ardhini. Na makombora ya angani bado yameelekezwa kwenye Nishati na Madini. Tayari kuanza kufyatuliwa muda ukifika.

Ndugu yangu Simbachawene awe na tahadhari kubwa. Akibaki amesimama upande wa wanyonge walio wengi, basi, ahesabu kuwa watakuwa nyuma yake hata pale atakapoelemewa na wachache wenye kujali maslahi yao.

Hivyo, chonde Simbachawene, usiende Nishati Na Madini ukageuka kuwa ' Simba wa Makaratasi!"

Maggid Mjengwa,

Dar es Salaam.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye5OqrGwonrkFGBV%3D9zBkjkodVnGDhtnvxDuriCSHm3%2Bow%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments