Hatimae tumbili yamng'oa AG, Nakumbuka bungeni AG aliwahi kutaka kutembeza makonde kwa Mh. David Kafulila na kumwita TUMBILI baada ya kafulila kumlalamikia kuhusu matumizi mabaya ya akaunti ya Tegeta Escrow. Baada ya tukio hilo la aibu hakuchukuliwa hatua wala kuonywa na chombo chochote si utawala wa Bunge wala serikari. Ni aibu mtu mheshimiwa sana na Jaji anae jua sharia za nchi zinazo zuia matusi hadharani, Hata bungeni kanuni zinazuia si matusi pekeyake hata lugha za kuudhi tu zinazuiliwa. Iweje kwa mwanasheria tena jaji mwenye dhamana kubwa serikarini amwite mwenzake tumbili? Sasa TUMBILI ni nani na MWANADAMU ni nani? Mwongo ni nani na MKWELI ni nani? Mbona aliyejiita mkweli sasa kakubali kuwa alikuwa anadanganya? UNAWEZA KUWADANGANYA WATU WOTE KWA MUDA MCHACHE LAKINI HUWEZI KUWADANGANYA WATU WOTE MUDA WOTE ndo historia ya walimwengu.
Nampa pole mwanadamu msomi sana na mwadilifu sana kuumbuliwa na tumbili.
0 Comments