Maoni Ya Baraza Juu Ya Ombi La TPDC La Kutaka Kuidhinishiwa Bei Ya Kusindika Na Kusafirisha Gesi Asilia
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Maji na Nishati (EWURA CCC) lilianzishwa chini ya kifungu namba 30 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA Act), Sura ya 414. Madhumuni ya Baraza ni kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA ambazo ni Majisafi & Majitaka, Umeme, Petroli na Gesi Asilia.
Kufuatia ombi la TPDC la kutaka kuidhinishiwa bei ya kusindika na kusafirisha gesi asilia, Baraza limechambua kwa kina ombi hilo na yafuatayo ni maoni yake:-
Makadirio ya gharama za mradi na ambazo zimetumia kukokotoa bei (tariff) zimekuzwa kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi na TPDC. Hata hivyo ni wazi kwamba gharama kubwa za uendeshaji, utekelezaji n.k. zinachangia bei ya gesi kwa watumiaji kuwa kubwa. Kwa vyovyote vile gharama hizi ni kubwa kupita maelezo (unrealistic) na Baraza linachukua fursa hii kuiomba EWURA (mdhibiti) kuzipitia na kuzihakiki ili kuepuka kuingiza gharama zenye utata kwenye "tariff". Kwa mfano, baadhi ya gharama hizo kwa Makao Makuu peke yake (kwa mujibu wa wasilisho la TPDC) ni kama ifuatavyo:
Huduma za kisheria Sh. 600 milioni,
Bima za magari (ya makao makuu) Sh. 300 milioni,
Matangazo, magazeti Sh. 150 milioni,
Gharama za kukirimu wajumbe wa Bodi ya Menejimenti (hospitality) Sh. 406 milioni,
Mikutano ya Bodi Sh. 700 milioni,
Mikutano ya Kamati za Bodi Sh. 600 milioni,
Gharama za Bodi ya Manunuzi (Tender Board meetings) Sh. 600 milioni,
Gharama za michakato ya kuajiri (recruitment cost) Sh. 400 milioni,
Kuegesha magari (Car park) makao makuu Sh. 300 milioni,
Gharama ya huduma za vyakula (cartering services makao makuu) Sh. 2 bilioni,
Zawadi, mahusiano (donation, gifts/public relations) Sh. 3 bilioni,
Gharama za kuomba tariff EWURA Sh. 270 milioni,
"Public Relations and Promotions" Sh. 625 milioni.
Rambi rambi na maziko ya watumishi, familia (staff welfare) Sh. 300 milioni, n.k.
Gharama nyingine zinazozua maswali mengi kuliko majibu na ambazo zimeingizwa kwenye "tariff" ni za mafunzo (training) kwa Watumishi. Kwa mfano, baadhi ya gharama hizo (kwa watumishi wa Makao Makuu) ni kama ifuatavyo:
Mafunzo ya muda mrefu nje ya nchi kwa mwaka kwa wafanyakazi 10 ni Sh. 1,620,000,000, sawa na Sh. 162 milioni kwa kila mtumishi,
Mafunzo ya muda mfupi nje ya nchi kwa wafanyakazi 10 Sh. 576 milioni, sawa na Sh. 57.6 kwa mtumishi mmoja,
Mafunzo ya muda mrefu (ndani ya nchi) kwa wafanyakazi 30 Sh. 1,728,000,000, sawa na Sh. 57.6 milioni kwa mtumishi,
Mafunzo ya muda ya mfupi, wiki 2 (ndani ya nchi) kwa wafanyakazi 30 Sh. 810,000,000, sawa na Sh. 27 milioni kwa mtumishi mmoja.
Eneo jingine lenye utata kwenye ombi hili la bei ni mishahara iliyopendekezwa. Mishahara inayopendekezwa ni mikubwa. Utetezi wa TPDC kuwa viwango hivyo vya mishahara ni kwa mujibu wa soko la ajira kwenye sekta za mafuta na gesi haujitoshelezi kwa sababu hauelezi soko hilo ni kwa nchi zipi. Kwa mfano mishahara inayopendekezwa ni kama inavyoonyeshwa kwenye mabano:-
Mkurugenzi Mkuu (Sh. 36,000,000/-),
Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo (Sh. 28,000,000),
Mameneja (Sh 21,600,000),
Maofisa waandamizi (Sh. 16,200,000) ,
Maofisa (wahasibu, HR, Masoko, Ugavi)(Sh. 12,600,000),
Wahudumu, madereva, makatibu muhtasi (Sh. 5,400,000) ,
Mbali na mishahara hiyo mikubwa, watumishi watapata stahiki nyingine kama bonasi, "mileage", bima ya maisha (life insurance), posho ya nyumba, huduma zingine k.m kulipiwa bili za maji, umeme, simu (utilities) n.k...
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments