Na Happiness Katabazi
KASINGE ni neno linalotumiwa watu wa Kabila la Wahaya wanaotokea Bukoba Mjini,Bukoba Vijijini na Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ambapo,Mwanamke wa Shoka ,msomi wa Kiwango Cha Juu wa ngazi ya Kimataifa amabye ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ni Mhaya.
Neno Kasinge hutumika kumwambia mtu aliyefanya jambo fulani ambalo wewe umeliona jambo Hilo ni Zuri hivyo umshukuru kwa kumwambia Kasinge.
Leo namwambia Nshomile, Profesa Tibaijuka ambaye ni Mwasisi wa Baraza la Wanawake (BAWATA) ambalo lilitikisa nchini enzi zile za Utawala wa serikali awamu ya Tatu hadi kufikia Mwanasheria Mkuu wa serikali kulipinga mahakamani, kwa msimamo wake aliouonyesha jana katika Mkutano wake na waandishi wa habari na alisema;
' Yeye msomi mwenzake Profesa Sospeter Muhongo ni majembe ya Baraza la mawaziri na ajihudhuru ng'o Kwani Haoni Sababu ya kufanya hivyo.Minamuunga mkono Kwani Hana kosa alilolitenda na msimamo wangu ndiyo huo siku zote.
Tena ' Nshomile' Tibaijuka umenikosha Katika Moja ya sentensi yako ambayo umesema hata Mungu aliwapa nafasi ya kujieleza Adamu na Eva Katika Bustani ya Edeni walipotuhumiwa.
Nasema umenikosha Kwani Katika makala yangu ya wiki iliyopita nilitaka watuhumiwa wa Escrow Wapewe haki Yao ya Msingi ya kusikilzwa Kwani hata Mungu alimpatia Eva na Adamu haki hiyo ambayo sisi wasomi wa Sheria tunaiita ' Right to be heard'.
Makala yangu hiyo ilikuwa na kichwa Cha Habari kisemacho: KIKWETE USIWASIKILIZE ' BUSH LAWYER KATIKA ESCROW'.
Nshomile m Tibaijuka ,kwa maelezo yako ya Jana naimani hata wale mabongolala wa Sakata la Akaunti ya Escrow watakuwa wameanza kukueleza.Maana nchi hii kuna baadhi ya watu yaani ni mabongolala wanajadili mambo wasiyoyajua uhalisia wake na wanawahukumu watu bila hatia.
Nshomile Tibaijuka, achana na mabongolala yaani watu wasiyo na akili na wana ajenda zao chafu za siyo tu za Kukupaka matope pia Profesa Muhongo na serikali pia isitawalike kwa Amani.
Songa Mbele ,na minaamini muda Si mrefu mabongolala ,wazandiki ,wazushi na Wapika majungu kuhusu Akaunti ya Escrow wataumbuliwa hadharani.Imefika zamu Yao kuvuliwa nguo hadharani. Kasinge mno Nshomilie Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, Omukama akubele.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Disemba 19 Mwaka 2014.
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments