Ndugu zangu habari za leo na hongereni kwa shughuli zenu za kila siku ili kujiletea maendeleo.
Ndugu zangu napenda kuwakumbusha juu ya zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kama ambavyo limetangazwa kwenye vyombo vya habari mbalimbali, zoezi hili na la majaribio katika maeneo yaliyotajwa hapo juu.
Ndugu zangu naomba tutumie nafasi hii vizuri sana kwa kuhamasisha watu hasa vijana wakajiandikishe kwa wingi na usahihi. Kama kuna kitu ambacho CCM wanatuzidi ujanja ni kutumia fursa hii vizuri kwa kupita nyumba kwa nyumba kuhamasisha wanachama wao wajiandikishe kwa wingi. Kwa hiyo nawasihi viongozi wetu wa SM waliochaguliwa hivi karibuni kutoka kwenye maeneo hayo tutumie nafasi hii vizuri. Pia viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA tumieni nafasi kwa kupita kwenye vijiwe na kuwachukua vijana wakajiandikishe ikiwezekana kupita kila siku kwenye vijiwe na kuwauliza kama wameshajiandikisha au la.
Pia wenye namba ya Halima Mdee mbunge wa Kawe tuwasiliane naye na kumkumbusha juu ya zoezi hili katika jimbo lake mama Susan Kiwanga huko Kilombero. Najua wanafahamu kwa kina ila kuwakumbusha na kuwahimizq si kosa.
KUMBUKENI ZOEZI HALITARUDIWA KWA UPANDE WA MAENEO HAYO LIMEANZA TAREHE 15/12/2014 hadi 21/12/2014.
Ahsanteni ndugu zangu.
--Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAP%2B7qpo%3DwgBCD5h0xP3U9fHUbva%3DfOb2n4-xaZLJbsxV7AQ63A%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments