[Mabadiliko] Waziri Saada Salum Mkuya ulilidanganya bunge kwa faida ya nani?

Friday, December 12, 2014


JF

Wakati wa kikao cha bunge kilichopita sakata la fedha za akaunti ya ESCROW liliikuwa likitikisa kila kona ya nchi!

Wakati akichangia mjadala, mbunge David Kafulila aliibua tuhuma kuwa ufisadi wa ESCROW umeifanya Tanzania kukosa zaidi ya dola za kimarekani milioni 450 fedha za miradi ya maendeleo kwa Tanzania kutoka MCC maarufu kama MCC project.

Bila haya wala aibu waziri wa fedha bi Saada Salum Mkuya alisimama kwa kujiamini mbele ya bunge na kudai kuwa MCC project imeshasainiwa na yeye mwenyewe na kwamba eti mwezi wa kumi na mbili (mwezi huu tulio sasa) fedha hizo zitatolewa kwa Tanzania tayari kuingizwa kwenye miradi ya maendeleo.

Jana tumeshuhudia balozi wa Marekani nchini Tanzania akiishinikiza serikali ya Tanzania kuwachukulia hatua wezi wote walioshiriki sakata la ESCROW ndipo MCC isainiwe.Hili likiwa ni tamko rasmi kwa Tanzania kutoka serikali ya Marekani.

Sasa waziri katika wizara muhimu inayoshughulikia uchumi wa nchi anapokuwa mwongo ili kulinda mafisadi na kuwa tayari kuwanyongelea mbali walalahoi sisi tumuoneje? Tumfananishe na kitu gani?

Watu wa aina hii kuwa nao katika dhamana tutasubiri sana kujikomboa na umasikini!

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACChgVRN9_zhLk8Ob9ifRhx_jTk1amc5j-21nJJbY1kCtEOHkA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments