[Mabadiliko] TPDC NA UKOKOTOAJI BEI YA GESI

Tuesday, December 16, 2014
Tayari wamekwisha anza. Maumivu ya kichwa huanza polepole

Maoni Ya Baraza Juu Ya Ombi La TPDC La Kutaka Kuidhinishiwa Bei Ya Kusindika Na Kusafirisha Gesi Asilia

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Maji na Nishati (EWURA CCC) lilianzishwa chini ya kifungu namba 30 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA Act), Sura ya 414. Madhumuni ya Baraza ni kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA ambazo ni Majisafi & Majitaka, Umeme, Petroli na Gesi Asilia.
Kufuatia ombi la TPDC la kutaka kuidhinishiwa bei ya kusindika na kusafirisha gesi asilia, Baraza limechambua kwa kina ombi hilo na yafuatayo ni maoni yake:-

Makadirio ya gharama za mradi na ambazo zimetumia kukokotoa bei (tariff) zimekuzwa kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi na TPDC. Hata hivyo ni wazi kwamba gharama kubwa za uendeshaji, utekelezaji n.k. zinachangia bei ya gesi kwa watumiaji kuwa kubwa. Kwa vyovyote vile gharama hizi ni kubwa kupita maelezo (unrealistic) na Baraza linachukua fursa hii kuiomba EWURA (mdhibiti) kuzipitia na kuzihakiki ili kuepuka kuingiza gharama zenye utata  kwenye "tariff". Kwa mfano, baadhi ya gharama hizo kwa Makao Makuu peke yake (kwa mujibu wa wasilisho la TPDC) ni kama ifuatavyo:
Huduma za kisheria Sh. 600 milioni,
Bima za magari (ya makao makuu) Sh. 300 milioni,
Matangazo, magazeti Sh. 150 milioni,
Gharama za kukirimu wajumbe wa Bodi ya Menejimenti (hospitality) Sh. 406 milioni,
Mikutano ya Bodi Sh. 700 milioni,
Mikutano ya Kamati za Bodi Sh. 600 milioni,
Gharama za Bodi ya Manunuzi (Tender Board meetings) Sh. 600 milioni,
Gharama za michakato ya kuajiri (recruitment cost) Sh. 400 milioni,
Kuegesha magari (Car park) makao makuu Sh. 300 milioni,
Gharama ya huduma za vyakula (cartering services makao makuu) Sh. 2 bilioni,
Zawadi, mahusiano (donation, gifts/public relations) Sh. 3 bilioni,
Gharama za kuomba tariff EWURA Sh. 270 milioni,
"Public Relations and Promotions" Sh. 625 milioni.
Rambi rambi na maziko ya watumishi, familia (staff welfare) Sh. 300 milioni, n.k.
Gharama nyingine zinazozua maswali mengi kuliko majibu na ambazo zimeingizwa kwenye "tariff" ni za mafunzo (training) kwa Watumishi. Kwa mfano, baadhi ya gharama hizo (kwa watumishi wa Makao Makuu) ni kama ifuatavyo:
Mafunzo ya muda mrefu nje ya nchi kwa mwaka kwa wafanyakazi 10 ni Sh. 1,620,000,000, sawa na Sh. 162 milioni kwa kila mtumishi,
Mafunzo ya muda mfupi nje ya nchi kwa wafanyakazi 10 Sh. 576 milioni, sawa na Sh. 57.6 kwa mtumishi mmoja,
Mafunzo ya muda mrefu (ndani ya nchi) kwa wafanyakazi 30 Sh. 1,728,000,000, sawa na Sh. 57.6 milioni kwa mtumishi,
Mafunzo ya muda ya mfupi, wiki 2 (ndani ya nchi) kwa wafanyakazi 30 Sh. 810,000,000, sawa na Sh. 27 milioni kwa mtumishi mmoja.
Eneo jingine lenye utata kwenye ombi hili la bei ni mishahara iliyopendekezwa. Mishahara inayopendekezwa ni mikubwa. Utetezi wa TPDC kuwa viwango hivyo vya mishahara ni kwa mujibu wa soko la ajira kwenye sekta za mafuta na gesi haujitoshelezi kwa sababu hauelezi soko hilo ni kwa nchi zipi. Kwa mfano mishahara inayopendekezwa ni kama inavyoonyeshwa kwenye mabano:-
Mkurugenzi Mkuu (Sh. 36,000,000/-),
Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo (Sh. 28,000,000),
Mameneja (Sh 21,600,000),
Maofisa waandamizi (Sh. 16,200,000) ,
Maofisa (wahasibu, HR, Masoko, Ugavi)(Sh. 12,600,000),
Wahudumu, madereva, makatibu muhtasi (Sh. 5,400,000) ,
Mbali na mishahara hiyo mikubwa, watumishi watapata stahiki nyingine kama bonasi, "mileage", bima ya maisha (life insurance), posho ya nyumba, huduma zingine k.m kulipiwa bili za maji, umeme, simu (utilities) n.k...Soma Habari Kamili »
Haki na Wajibu Wa Mtumia Huduma
Ili kuwepo na ufanisi katika utoaji wa huduma za maji na nishati, ni sharti mtumiaji awe na uelewa
wa haki zake kwenye huduma anayopewa.. more »
Vidokezo kwa Mtumiaji wa Huduma ya Maji
Kwa matumizi bora ya maji tunaweza kusaidia kuhifadhi vyanzo vya maji kwa vizazi vijavyo. Kumbuka kila tone lina thamani. Bonyeza hapa kupata vidokezo muhimu kwa mtumiaji wa huduma ya majimore »
Vidokezo kwa Mtumiaji wa Nishati ya Petroli
Kuna njia za kufanya fedha zako kuwa na thamani zaidi kwa kila lita ya petroli utakoyonunua au kutumia. Bonyeza hapa kupata vidokezo muhimu kwa mtumiaji wa bidhaa za petroli. more »
Mchakato wa Kushughulikia malalamiko
Baraza linatambua kuwa kila tatizo unalokuwa nalo la huduma ya nishati na maji ni nyeti na linahitaji ufumbuzi.more »
Vidokezo kwa Mtumiaji wa Nishati ya Umeme
Utumiaji wako mzuri wa umeme ni moja ya njia za haraka za kupunguza bili yako ya nishati. Bonyeza hapa kupata vidokezo muhimu kwa mtumiaji wa huduma ya umeme more »
Mafanikio ya Baraza
Toka kuanzishwa kwake, Baraza limetekeleza shughuli mbalimbali zinazolenga kufikia dira na dhamira ya uundwaji wa Baraza

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAGFQo2QSrT7CK7awLQQG23GHDU%2B-OXA8xSRyo_%3Df%3DEaJXOt6rA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments