KWAKO DADA/ BINTI/ MWANAMKE
1. Usipokee zawadi bila kuhoji madhumuni ya mtoaji… kuna wanaume hawajui kueleza hisia zao na wapo wanaoamini mwanamke mpe zawadi…mpe pesa utampata tu pasipo kujieleza….. Hivyo anapokupa zawadi ndio anakujulisha hisia zake. Unapozipokea na kushukuru, kwake yeye inamaanisha umemkubali…. Kuwa wazi tu umuulize madhumuni yake ili baadaye akikugeuka umsute kwa maneno yake mwenyewe!!.... unatumiwa vocha, vijichenji kwenye Mpesa… unachekelea tu weeee!!
2. Unapokwenda kuonana na mtu kwa mara ya kwanza na mtu mwenyewe hufahamu kazini kwake, hujui hata ukikutwa na tatizo utaanzia wapi… hakikisha una usafiri wa kukufikisha eneo la makutano na usafiri wa kukuondoa eneo hilo kurudi kwako….Kamwe! usipande gari lake au taksi pamoja naye!.... eti nikupe lifti nikushushe hapo mbele…Sura sio roho.weeee!
3. Jilipie chakula na mazagazaga mengine utakayotumia!.... usiende kukutana na mtu ukiwa mifuko mitupu!.... ujinga huu usiuthubutu… kubali tu endapo atasisitiza sana juu ya hilo! Vinginevyo gharamikia sehemu yako au yote ukiweza hata kama ni maji ya kunywa!... kwa kulipia soda moja na tusambusa tuwili usishangae mtu akakuletea inshu za kuondoka wote!
4. Usitumie kilevi, au kitu chochote kigeni wakati wa makutano na mtu usiyemfahamu vyema…. Usiogope kuonekana mshamba, wakati mwingine ushamba unaweza kukuepusha na matatizo!
5. Unapoanza kujenga urafiki na mtu mgeni… usiombe vitu vidogo vidogo…hela ya kula, hela ya vocha…. Have some dignity lady!... wapenzi/ waume zetu tunawatandika mizinga huu ni msalaba wao lakini mwanaume asiyekuhusu na ndio umemfahamu hata mwezi hamjamaliza…hapana! Jiheshimu aisee!... tamaa yako ndogo tu inaweza kukuingiza kwenye majuto makubwa sana maana unavyojiweka ndivyo mwanaume atakavokuchukulia!.... after all!...usingekutana naye ungetoa wapi hela ya kula au vocha?! Vinginevyo uwe tayari pia kuliwa kama unavyokula!
6. Kutana naye sehemu ya wazi…. Restaurant!... sio mtu anakwambia njoo kwangu… au nimefikia hotelini njoo chumba namba fulani… ni mbuzi pekee ataingia chumbani kwa mwanaume na akili ya kuwa hatoguswa…. Ukishakubali kukaa faragha na mwanaume jua lolote laweza tokea…. Sasa kama hauko tayari unaenda faragha kufanya nini?!!...mwanaume atakwambia sitakugusa kwa kujiapiza na miungu ya kwao…ingia mtegoni uone viapo vilipo…utajuta!!.... kuwa na msimamo binafsi!
7. Usibebe kundi la watu kwenye miadi ya kwanza…. Huu ni ushamba jumlisha ujinga!...kama unataka ulinzi au kumthaminisha na nini na nini….watangulie wakae mahali kisha uingie. mezani pale mkae wawili tu…. Unaweza kuja na mtu kama tu umemfahamisha mhusika juu ya hilo….kuna watu wana uchungu na hela zao …anavyogharamika ndivyo anavyopanga kukukomesha!....mbaya zaidi mnakuja mikoba mitupu…shame on you!
8. Mjulishe mtu mmoja ukweli wa mahali unapokwenda na nani unaenda kukutana naye ndio maana tuna partners in crime LOL!!. Hili ni jambo muhimu sana, huwezi jua linalokuja. Mara zote fanya hivi na lolote likitokea watu watajua pa kuanzia. Kuna wagonjwa wa akili wanavaa suti siku hizi…shauri yako! Hata kama utawaambi watu wote unaenda Sinza…mtu mmoja anapaswa kujua kuwa ukweli unaenda Buzaaa!
9. Usiwe mwepesi KUAMINI WATU na kujenga urafiki wa karibu saaana na watu ovyo ovyo…hasa watu wa mitandaoni…jifunze kutofautisha marafiki na kampani… kwasababu anakuchekea sana, au anaonekana muungwana sana, au anakuinbox sana ghafla ameshakuwa shost!... ushamkaribisha kwako, ushamuacha akukocontrol… wanawake wa sasa sio wazamani shost!... wengine wako kazini!
….kule kutokumjua vizuri hakuondolewi na chatting za inbox… Jifunze kurudi nyuma hatua moja na kumsoma mtu! … hii ni iwe rafiki mwanaume au mwanamke… weka distance fulani ujiridhishe kwanza, na usiruhusu mtu usiyemjua akujue wewe kwa undani!
10. Mwisho! Kutongozwa sio dhambi… ni sehemu ya maisha ya mwanamke!... lakini haimaanishi kila anayekutongoza umsikilize, uonane naye, uamini kuwa anakupenda kweli, ujione una bahati ama ndio utake kujaribu kama mtafikia ndoa…NO!... kuna wakati wanaume huamua tu kucheza na akili yako… na ukute ni watu wanao bet kabisa nani atampata huyu!...
Usiangalie profile ya ukaona picha za suti mbili tatu… post za maana nyiiingi na blah blah blah zingine …ukanusa harufu ya pesa…buzi hilooo…weeee! … chunga sana! Hakuna pesa nyepesi toka mwanaume!! HAKUNA!! ....chakarika!
Ukiona watu wajengewa majumba au wananunuliwa magari au wanatunzwa… uliza kwanza upewe ramani…uonyeshwe njia… sio kudaka daka watu ovyo ukitarajia mteremko…. Utakwenda siku si zako!
Mwanamke!... msichana! Dunia imeharibika… kuna watu wanatafuta viungo vya binadamu, kuna watu wanafanya kazi ya kuviuza, kuna watu wana matatizo ya akili…. Kuna watu ambao ukimkatalia anachotaka mkiwa faragha anaweza kukuua…
kuna hatari chungu nzima hapo nje…. Kabla hujachukua hatari moja na kuijaribisha hakikisha umejiridhisha kuwa ni hatari isiyoweza kugharimu maisha yako!!
natumaini kuna la maana japo moja katika upuuzi wote huu Lol!
Nikutaki siku njema
LAURA PETTIE
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments