[wanabidii] KUAHIRISHWA KWA MDAHALO WA KATIBA TAREHE 16 JUMAPILI NOVEMBA 2014

Saturday, November 15, 2014

TAARIFA KWA UMMA: KUAHIRISHWA KWA MDAHALO WA KATIBA TAREHE 16 JUMAPILI NOVEMBA 2014.

Kwa niaba ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere napenda kuwatangazia kwamba Mdahalo wa Katiba uliokuwa ufanyike Jumapili tarehe 16 Novemba umeahirishwa na utafanyika siku chache zijazo. Taasisi ya Mwalimu Nyerere itatoa taarifa juu ya Ukumbi, siku, saa ya Mdahalo wa Katiba utakaofuata kwa hapa Dar es Salaam kufuatiwa kuvurugwa kwa Mdahalo wa Katiba siku ya Tarehe 2 Novemba 2014.

Taasisi inawasihi watanzania na wenye mapenzi mema na Mchakato wa Kupata Katiba Mpya kuendelea kuwa na subira, ustahimilivu na kuendelea kujadiliana kwa hoja na sababu na kujielimisha juu ya Maudhui ya Mchakato ambayo ni pamoja na Katiba ya Mwaka 1977, Rasimu Ya Katiba Toleo la Pili na Katiba Inayopendekezwa.

Mwisho, Taasisi ya Mwalimu Nyerere inawapa pole na kuwaomba radhi wale waliokuwa wamejiandaa kuja Jumapili hii, kujifunza juu ya Mchakato wa Katiba na Katiba Inayopendekezwa.

Asanteni na ninaomba tuusambaze ujumbe (SHARE) juu kwa watanzania wengi zaidi huku tukijiandaa na Mdahalo wa Katiba siku chache zijazo.

Humphrey Polepole.
Mdau wa Maendeleo

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments