[wanabidii] Hatimaye Siri ya Ziara ya Lowassa Nje ya Nchi yabainika

Tuesday, November 25, 2014
Nikiwa natokea Dar es salaam kuelekea Dodoma jana mchana, tayari kwa kufuatilia mjadala wa bunge juuya Ripoti ya CAG kuhusu account ya ESCROW inayotarajiwa kusomwa siku ya jumatano, kuna taarifa nilizipata kutoka kwa moja ya washauri wakubwa wa Edward Lowassa ambaye nilibahatika kupanda naye gari moja (kwa sababu za kiusalama naomba nisitaje jina lake). Inasemekana kuwa Edward Lowassa na kambi yake wamegundua kuwa mipango yake ya kutaka kutumia Ripoti ya IPTL kuiangusha Serikali na hasa kumuhusisha Waziri Mkuu kwenye kashfa hili Imegonga mwamba baada ya kibaraka wake Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai kuondolelewa katika kuongoza vikao vya Bunge na kupewa likizo ya muda wa siku 14 nchini Ufaransa. Taarifa zinasema kuwa baada ya maamuzi hayo Lowassa amekuwa kwenye wakati mgumu sana kwani hiyo ndiyo ilikuwa Karata yake ya Mwisho katika kujitengenezea njia ya Urais mwakani 2015.

Kambi ya Lowassa inaamini kuwa uwepo wa Spika Anne Makinda ni pigo kubwa kwake kwani Spika huyo amekuwa imara mara zote anapoendesha vikao vinavyojadili mambo mazito yanayogusa maslahi ya Taifa bungeni na haingiliki kirahisi tofauti na Job Ndugai ambaye wazi ameonyesha mahaba yake kwa Lowassa kwa kuahidiwa Uspika pindi Lowassa atakapokuwa Rais. 
Tayari kuna taarifa kuwa mwanamkakati mkubwa na Master Mind wa Safari ya Matumaini ya Lowassa, Mtemi Andrew Chenge ametajwa kuhusika kwenye kufanikisha dili la IPTL wakati akiwa Mwanashria Mkuu wa Serikali. Hili linathibitishwa na Chenge mwenyewe ambaye amekiri kupokea zaidi ya Bilioni Moja na nusu kama Consultancy fee. Hali hii imepelekea kambi ya Lowassa kuandaa mikakati mizito ya kumnasua Chenge katika sakata hili. Tayari hadi muda huu takribani bilioni 4.5 imetumika kwa ajili ya kushawishi wabunge wa CCM na upinzani kushinikiza Pinda ajiuzuru kwa kashfa hii.

Kufuatia kuondolewa kwa Ndugai kuendesha vikao vya bunge vinavyoendelea Dodoma na kuelekea Ufaransa, tayari Waziri Mkuu alijiuzuru kwa kashfa ya Ufisadi ya Richmond jana alifanya safari ya ghafla nje ya nchi kuelekea Ujerumani lakini taarifa za ndani zinasema, Lowassa haendi Ujerumani anaenda Ufaransa kufanya kikao na Job Ndugai kuona ni kwa namna gani wanaweza kufanikisha Waziri Mkuu anadondoka na kashfa hii.

Hali ni tete hadi muda huu Mjini Dodoma wabunge wanaonekana kujipanga makundi huku kundi linalompigia Chapuo Lowassa wakiwa na hofu kubwa kuwa mkakati wao umevuja na wamegonga mwamba wakati wabunge wengi wa CCM wameonyesha kuchoshwa kwa kuyumbishwa na wasaka Urais wenye tuhuma za ufisadi na wafanya biashara walionyimwa vitalu na wabunge wengi wamejipanga kesho kutema nyongo na kusema ukweli kuhusu IPTL.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments