Re: [Mabadiliko] RE: [wanabidii] JAJI WARIOBA APECHE ALOLO

Sunday, November 09, 2014
Yupo tena anawasoma vizuri tu.
em

Sent from my iPhone

On Nov 8, 2014, at 7:26 PM, Shigela Aloyce <comrshigela@gmail.com> wrote:

Nico,

Mwalikeni dada Katabazi hapa jukwaani, kama yupo naomba nijulishwe tafadhali!

SA.

On Nov 8, 2014 9:04 PM, "'Leila Sheikh' via Mabadiliko Forum" <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:
Ooh!
Shukran

Leila Sheikh

On 8 Nov 2014, at 20:42, "'jabir yunus' via Mabadiliko Forum" <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:

Dada Leila nawe! Apeche alolo ni mtu hohehahe, muflisi kipesa/akili/fikra.
 Sasa huyo ndo Joseph Sinde Warioba.

J
From: Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Saturday, November 8, 2014 6:54 PM
Subject: RE: [Mabadiliko] RE: [wanabidii] JAJI WARIOBA APECHE ALOLO

Hahah hii mimba inaleta kichefu chefu well mzuri kasema wacheni.blah blah weka No maisha yasonge
On Nov 8, 2014 8:38 AM, "Nicomedes Kajungu" <nicomedes76@gmail.com> wrote:
Huyu dada atawaua na vichefuchefu
On 8 Nov 2014 14:55, "'Ambokege Benard M' via Mabadiliko Forum" <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:
Hii makala inatia kichefuchefu!


ABM
From: 'Leila Sheikh' via Mabadiliko Forum
Sent: 11/7/2014 9:05
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Subject: Re: [Mabadiliko] RE: [wanabidii] JAJI WARIOBA APECHE ALOLO

Den
Apeche apolo maana yake nini?

Leila Sheikh

On 7 Nov 2014, at 7:42, denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> wrote:

Huyu dada ameamua.......
On Nov 7, 2014 1:33 AM, "Azaveli Lwaitama" <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com> wrote:
Ndugu Muganda,
Andiko la Katabazi linakupa picha nzuri za "busara" za kakundi ka kihuni kalikokiteka chama cha CCM na kanapanga kunedelea kuwatawala Watanzania kibabe. Nimesoma kwa makaini andiko la Katabazi na ni "zuri"...Andiko linagusia hata na kazi nzuri iliyofanywa na jamaa wale waliomteka na kutesa Dr Stephene Ulimboka na unapata picha kuwa lengo kwa siku ile pale Ubungo Plaza lilikuwa ni "kumlimboka" Jaji Warioba na wenzake kama kipindi kile live kingeendelea kurfishwa "live" . Sasa inatazamia kuwa njia hizo za kumziba mdogo jaji Warioba na wenzake hazitaitajika kutumika maana Rais yetu mpendwa Prof Dr. Kikwete ametoa nasaha kuwa midahalo kama hule wa ubungo Plaza hisitishwe kwa sasa hadi hapo baadaye, mwezi mmoja kabla ya kura ya maoni. Andiko la Katabazi ni zuri linatufungua macho nchi inavyotawaliwa na yeye bila shaka alikuwa anatekeleza majukumu yake. Kadiri mwisho wa utawala wa kifashisti   wa kakundi ka wahuni kalikokiteka chama cha CCM unavyonukia kakundi haka katatenda mambo mengi ya kinyama kwa imani kuwa matendo haya ya kinyama, kwa  kumsaada wa watawala wa Janhuri ya Watu wa China , yataepusha mwisho huu!!! Vitisho na matendo kama yale ya kuteka na kuua vitaongeza  kadri mwisho wa ufashisti huu utakavyo karibia!!! Tunshukuru sana Katabazi kwa elimu aliyotoa katika andiko lake!! Bahati mabay kwake na watu wa aina yake ni kuwa hata tukiuawa  au kujeruuiwa wakorofi  wangapi, mwisho wa ufashisti Tanzania HAUEPUKIKI  NA AKINA KATABAZI ipo siku matendo na maneno yao ya nitisho na mauaji yaliyolenga kunyamazisha mawazo mbadala yatawarudia  na kuwatafuna!! Ukweli  na haki vitashinda hata kama tutaumizwa na kufa wengi kabala ya ushindi huo!!!
Mwl. Lwaitama

Date: Thu, 6 Nov 2014 10:39:56 -0500
Subject: Re: [wanabidii] JAJI WARIOBA APECHE ALOLO
From: emuganda@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Hivi ninyi bado mnapoteza muda wenu kumsoma Katabazi? Huyu anajikweza anadhani ataongezewa cheo. Apache alolo mwenyewe.
em

2014-11-06 7:30 GMT-05:00 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>:
Nimesoma hii makala kusema.kweli huyu.muandishi.amefanya kazi nzuri.saana kwa wanaomtuma. Nakubaliana nae kabisa kuwa.mzee Warioba kafirisika kisiasa na kifikira ila nisingependa kumuhukumu haraka bila.kumuhukumu mfirisika.namba moja aliempa hiyo kazi.
Lazima uwe na tatizo kidogo mpaka umteue mtu apache alolo kukifanyia kazi nyeti kes taifa hili. Na kwa mwendelezo.huo huyu mpumbavu anaeandika hii habari hakuweza kuiona hiyo mantiki anaongelea final.product hii ni higheet degree ya ujuha tulionayo na bahati.mbaya mijuha.kama.hii inapata.nafasi kwenye sehemu.zetu za kueleimisha jamii.
Jaji warioba na ufirisika wake wa nini vile sijui amebeba mawazo ya wananchi hana pendekezo pale hiyo tume ya wenye bongo.shibe inakaa kwenye vikao na kutoa inayofikiria yanawafaaa wananchi.
Ni kweli itapita lakini sijui huyu muandishi anasoma.anachoandika.au anaandika tu. Unawezaje kutonyesha live kuwa itapitishwa kibabe hiyo katiba na unataka tushangilie
On Nov 6, 2014 1:59 AM, "Oksana Spice" <worldngojobs@gmail.com> wrote:
JAJI WARIOBA APECHE ALOLO 
Na Happiness Katabazi
APECHE ALOLO ni Msemo ambao ulikuwa ni maarufu sana Katika Miaka ya 1990- 2000 Dar es Salaam. Msemo huu ulikuwa ukipendwa kutumiwa na 'watoto wa mjini' ambao walikuwa wakimaanisha Kuwa mtu Fulani HIvi sasa amefirisika kifedha, sera,Hana dira wala mwelekeo, Hana Mpango wowote. Hivyo ambaye alikuwa Hana Fedha,Hana sera walikuwa wakimuita mtu Huyo ni Apeche Alolo.
Hivi sasa watoto wa mjini wanatumia msemo huu Kuwa 'Fulani amefulia' , Shoka Moja Mbuyu chini, Choka Mbaya, kwishineiiii.Wana maanisha Mtu Fulani amefirisika kifedha, sera Hana dira wala mwelekeo na Hana lolote.
Nimelazimika kutumia neno Hilo kwasababu Oktoba 2 Mwaka huu ,ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam, kulizuka vagi hali iliyosababisha mdahalo wa kuzungumzia Katiba mpya uliokuwa imeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuvunjika na mgeni Rasmi ambaye ni aliyekuwa Mwanyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba ambaye aliishia kukutwa na wakati mgumu na kudhalilika kutokana na vurugu hizo.
Kwa zaidi ya Miezi Tisa sasa aliyekuwa Jaji Warioba baada ya kumaliza kazi yake hiyo aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete, jina lake lilikuwa likibeba uzito wa juu Katika vyombo Vya Habari.
Jaji Warioba Mbele ya baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa wa upinzani alionekana ni mtu jasiri na anayeipenda sana nchi yake kuliko wana CCM wenzake na Kana Kwamba Jaji Warioba ndiyo aligeuka Kuwa ni Kama mtu aliyepewa jukumu la kuwafundisha Watanzania Kuwa Katiba mpya ni lazima iwe na vitu ambayo Tume yake ilivipendekeza na baadhi ya watu walimchukulia Warioba kama ndiyo msemaji wa wananchi ,Nyakanga wa kuwafunda watanzania ya jinsi Katiba mpya inayakiwa iweje, na kweli Warioba aliona anapendwa na watu wote na kusikilizwa na kwamba yeye ana akili sana kuliko Watanzania wote.
Jaji Warioba alisahau maneno ya mwanamuziki Mwandamizi wa Bendi ya FM Academia, Mule Mule FBI , aliyoyatoa Katika Wimbo wa Ndoa ya Kisasa uliopo Katika Albamu mpya ya Bendi hiyo inayojulikana kwa jina la CHUKI YA NINI, ambapo Mulemule asikika Katikati ya Wimbo huo Kuwa ( Ukijua Kutendwa basi na ujue na Kutendwa).
Warioba Mtani wangu siku zote alifikiri ataendelea Kupendwa na wananchi anaowahutubia Katika midahalo na akasahu Kuwa ipo siku anaweza Kutendwa na kweli watoto wa kihuni ' watoto wa Mbwa' , Novemba 2 mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza, walimtenda .
Sisi Watu wa Kabila la Wanyambo tunaotokea Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera , uhuni aliofanyiwa Warioba tunasema ' Warioba Bamkora Kantu'. Yaani wahuni wamemfanyizia .
Inaniwia vigumu kuamini kuwa kutokana na fezea ile aliyoipata Warioba sijui kama atakubali kirahisi tena mialiko ya kushiriki kwenye midahalo ya kutoa maoni ya kupinga Katiba Pendekezwa.Naona sasa amekoma .
Na kama anafikiri sawa sawa na anawashauri wazuri na hawamuonei haya kama mimi mtani wake, watakuwa na ujasiri kama wangu wa kumweleza hivi kuwa hivi sasa Mtani wangu Warioba ni Apeche Alolo, anatakiwa atulie awe mtazamaji na ale pesheni yake kwa nafasi huku akisubiri siku za Kuitwa na Mwenyezi Mungu kule kwenye Makao yetu ya milele maana hapa Dunia sote sisi tunapita na niwapangaji.
Warioba ni Apeche Alolo kwasababu Tayari baadhi ya watu wameisha Choka kusikia maoni yake kuhusu Katiba Mpya Kwani wananchi wamebaini hata wakiendelea kumsikiliza maoni yake hayo hawawezi kuibadilisha Katiba Pendekezwa na baadhi ya wananchi wamekinai kumsikiliza Warioba kwasababu wabunge wao waliowachagua mwaka 2010 walikuwa ndani ya Bunge kwaniaba ya wananchi Hao wakawatungia Katiba Pendekezwa.
Sasa wananchi hao wanasema ni uwendawazimu kumsikiliza Warioba na kukubalina na mawazo yake kwasababu wao waliwapigia kura wabunge wao na bado wanaimani nao na ndiyo wabunge walienda kuwawakilisha Wapiga kura Hao Katika Bunge la Kutunga Katiba.
Hivyo Warioba ni Apeche Alolo, yaani kafirisika kisera na mawazo hivyo wanachokisubiria hivi sasa ni kuona sura mpya majukwaani zikiipiga kampeni kuhusu Katiba pendekezwa ili waweze kuipigia kura ya ndiyo au hapana. Maoni , mashati anayovaa Warioba ambayo Marehemu Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela alikuwa akipendelea kuyavaa wamechoka kuyaona Kwani ni Kama ya nawatetea kiungulia Kama siyo Kichefuchefu na yenye Lengo la kuleta vurugu nchini.
Lilokuwa Bunge Maalum la Katiba lilitumia madaraka yake iliyopewa kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2012 , ya kuboreshwa na kurekebisha ile rasimu ya Tume ya Jaji Warioba.
Kwa sisi tunaofuatilia mambo mbalimbali ya mustakabali ya taifa letu tulimshuhudia Jaji Warioba na wajumbe wa Chache wa Tume hiyo kila kukicha akitoa maoni yake ya kutaka bunge la Katiba lisitishwe, mara akidi ya wajumbe wa bunge lile haitatimia lakini akidi ikaja kutimia, anashangaa Mwenyekiti wa lilokuwa Bunge la Katiba , Samwel Sitta jeuri anaipata wapi,serikali Tatu hazikwepi.
Na Septem

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/D07B88BF-56E4-416A-B8CE-4FB0882CAB61%40yahoo.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAPPZ%3DWzS2N%3DpXnbRLKOfonv4Ciy7B1G5fKWoaUUZC7sgOim0rg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments