[Mabadiliko] MAKUBWA KAMA HAYA; RAIS NA IKULU KUTOJUA NI MZAHA MKUBWA KWENYE VITA DHIDI YA UFISADI

Thursday, November 27, 2014

Wanaoujua ufisadi wa IPTL katika ukubwa, mapana na urefu wake wanatambua kuwa kushughulika na Escrow Account pekee (kisha kujiaminisha tumeshughulikia IPTL katika ujumla wake) ni mzaha unaoweza kuvumiliwa kwa minajili ya kuacha muda au wakati uwe hakimu mzuri.

Lakini kwa wale wanaoujua undani wa IPTL namna mkataba wa kilaghai na kifisadi ulivyosainiwa tangu miaka ile ya 90 wakati nchi ilipoingia katika shida kubwa ya umeme, huku wahusika wakituingiza katika uvundo mkubwa ambao umezalisha matawi mengi, mojawapo likiwa ni hili la Escrow Account (cha mtoto?), watakuwa na maswali mengi hasa baada ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya PAC.

Mojawapo ya maswali hayo ni je;

Kweli kwa ufisadi mkubwa kama huu, ukiwa ni sehemu ya matokeo ya moja ya mikataba mibovu katika sekta ya nishati, kwamba mabilioni ya fedha yaliyochotwa sehemu nyeti kama benki kuu, yakagawiwa kwa kiwango kile, kiasi ambacho mtu anaweza kujenga hoja na kuhitimisha kuwa kulikuwa na elements za state capture or rather an institutionalized corruption, kwamba ofisi kuu ya nchi na mwenye ofisi ambaye kimamlaka ni Rais Mtendaji alikuwa hajui yote haya? Kwamba aliyekuwa anajua ni Waziri Mkuu pekee!

Tena usisahau kuwa kulikuwa na kauli 'tata' kutoka ikulu kuhusu suala hili hili, iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi

Lakini pia ukiisoma vyema ripoti ya PAC huoni neno hata moja likitolewa kama mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kwa Benki Kuu au Gavana! Hili linaibua utata mkubwa sana. Maana hapa kunaweza kuwa na clues...

Hapo hatujahoji kwa nini Wizara ya Fedha au watu wake pale hawajaguswa kabisa, wakati huo huo kuna maneno maneno kuhusu kifo cha Dkt. Mgimwa.

Kama hiyo haitoshi, tuliambiwa mapema tujiandae kupambana na facts si watu wakati ripoti itakapowasilishwa.

Suala la 'ukimya' kwa ofisi kuu ya nchi kwenye hili, it is a question which remained to be answered! Time will tell, alisema Bob.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMgDvukiDsjUZg_ng9Anbj%2BT%3DxhatkHBUMAPkoT_qZSESh2B%2BA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments