Obstat PrincipiisGAZETI CHANGAMOTO:
LUDOVICK: NINAFANYA KAZI YA CHADEMA.
Wiki iliyopita tuliona pamoja na mambo mengine kuwa kisha kupewa kadi ya chadema rasmi mwaka 2009 nilikuwa mwenyekiti wa kwanza wa CHASO DUCE. (chadema students organisation). kulikuwa tayari na base ya kutosha kutokana na mazingira yaliyoandaliwa tayari na baadhi ya watangilizi wetu hapo hawa akina Mtela Mwampamba na Gwakisa Mwakasendo. hawa wakifahamika kwa harakati zao katika siasa za vyuoni.nakumbuka Gwakisa alikuwa akitembelea campus ya mlimani uongozi wa huko walipiga simu DUCE kulalamika kuwa mtu wa DUCE amevamia mlimani. Ni jambo la kusikitisha kuwa wapambanaji hawa wote leo wamejiunga CCM. Nikiwa mwenyekiti wa CHASO tuliandaa ufunguzi wa tawi na dokta Slaa ndiye alikuja kulizindua. tangu wakati huo nikawa in some ways insider wa chama hasa kwa sababu ya mikakati ya mara kwa mara tuliyokuwa tunafanya kwa ajili ya chama chuoni. kama ada hilo liliniweka katika matatizo na uongozi wa chuo. mwaka uliofuata niliombwa kugombea urais wa serikali ya wanafunzi na kutokana na nguvu niliyokuwa nayo na ushawishi ilikiwa wazi kuwa niyachaguliwa kuwa rais. Vijana wa CCM wakisaidiwa na dean of students wa wakati ule Dr.Therezia Huvisa ambaye ndiye alikuwa mlezi wa CCM DUCE walifanya kila hila ili kuniengua. kwa kweli walishindwa kwa kila njama mpaka hatua ya mwisho wakamuomba Makamba akiwa Katibu wa CCM wakati huo awasaidie. kuna taarifa za kuaminika kuwa mzee makamba ndiye alitoa agizo kwamba basi wagombea wote wa urais waenguliwe nafasi itangazwe upya na walioenguliwa wasiruhusiwe kugombea tena. Na tukaenguliwa wote. lakini mgombea niliyemuunga mkono akawa na nguvu sana pia akafanyiwa mizengwe na mimi mwenyewe kwa maelekezo ya Theresia Huvisa nikakamatwa na auxiliary police na kuwekwa ndani hadi baada ya matokeo ya urais kutangazwa na mgombea wa CCM kupata ushindi. Wala haikuoshia hapo. hata viongozi wa serikali ya wanafunzi walipotofautiana bado Huvisa aliniandama mimi kiwa ndiyo ninachochea vurugu zile. katika kutapatapa huko ikasemwa kuwa Mwita Mwikabe alikuwa amekuja chuoni kwa mwaliko wangu. jambo hilo halikuwa kweli. bali kwa mshangao wangu na kwa kweli jambo hilo lilinishangaza sana Ally Chitanda akiwa kaimu mkurugenzi wa vijana taifa wa CHADEMA alikuja akitaka kuhonga tume ya uchaguzi ya chuo ili inipitishe. Na alikuja na kukaa hadharani na bila tahadhari yoyote akiongea. niliambiwa juu ya kikao kile na kupelekwa na mtu aliyeitwa Ndelwa mwanachadema aliyetokea mkoa wa mbeya akiwa kama mratibu wa mambo ya CHADEMA DUCE siku hizo. tume ya uchaguzi ilikataa rushwa ile wakisema wangefanya kazi zao kwa uadilifu bila mashinikizo ama ya CCM wala CHADEMA.niliogopa kuwa labda wangeniengua kwa sababu ya chama changu kutaka kutoa rushwa, lakini nawapongeza kuwa waliongozwa kweli na uadilifu angalau kwa kipimo hicho. japo sikuwa rais wa chuo lakini bado nilikuwa na ushawishi mkubwa na naweza kusema kuwa ni mimi na wenzangu ndiyo tulishawishi na kuinfluence uchaguzi wa rais aliyefuata na niliona aliganya vema sana kutetea haki za wanafunzi tofauti na kibaraka wa CCM aliyemtangulia. Aidha tukiwa katika vikao vya chaso nilitofautiana sana na vijana wengi hasa Juliana Shonza akiwa mwenyekiti wa umoja huo kwa vyuo vya Dar es salaam. Shonza na wenziye walikuwa wakipinga sana CHASO kuwa chini ya BAVICHA wakiona kiwa chaso ni wing ya wasomi kwa hiyo haikupaswa kuongozwa na BAVICHA. na hoja yao nyingine ilikuwa kudai chama kitoe nafasi ya ubunge kwa CHASO.ili kutimiza hayo wakataka kuandika katiba ya CHASO.nakumbuka kupinga mawazo yote matatu kuwa hatuna haja ya kuanza kujitenga na wing ya chama vijana wala kuwa na mawazo ya kiCCM kufai mkoa maalum wa vyuo vikuu. nilichukiwa. ni bahati mbaya kuwa hadi leo vijana wengi wa CHASO ni wapinzani wa BAVICHA na wanapokuja huko basi wanataka wapewe uongozi. uhusika wangu na CHASO kwa kweli uliletea matatizo shuleni. nikiwa kiongozi wa wanafunzi wakatoliki pia wana CCM walipenyeza siasa katika mambo ya kanisa. kupitia kundi la karismatiki ambalo nalo kama mwenyekiti wa wakatoliki nilikuwa nikigongana nalo mara kwa mara kutokana na baadhi ya itikadi zake zinazikiuka mapokeo ya kanisa, bila taarifa wala ruhusa ya chaplain yakaandaliwa mapinduzi kanisani. ikazushwa hoja kuwa nijiuzuru. Katika mazingira haya ya uadui wa kudumu na dokta theresia huvisa aliyekuwa dean wetu mpaka anaondoka kwenda bungeni, nilishangaa kusikia kuwa alisema eti mimi nilikuwa kijana wao yatima wakinilipia ada. ukweli ni kwamba kwa sababu yeye alikuwa mlezi wa CCM chuoni nami nikiongoza harakati za CHADEMA chuoni, tunaweza kusema kwa hakika kuwa huyu alikuwa adui yangu namba moja. maneno yake bungeni kuwa mimi nilikiwa kijana wao yalikuwa ni uongo mtupu na labda kama aliamua kujikosha kwangu kwa mabaya yote aliyonitendea ikiwa ni pamoja na kuniweka ndani. lakini siwezi kushangaa kwani mama huyu amekuwa hivyo yangu akiwa DUCE.
KUKUTANA NA LWAKATARE. Mwaka 2010 karibia na uchaguzi mkuu tulikuwa likizo. mimi nikiwa Bukoba niliamua kwenda kusaidia chama changu wakati wa uchaguzi mkuu. nilipokelewa ofisini na mwenyekiti wa chadema wilaya ya bukoba mjini na wakati huo ndg.Sherejei na katibu wake Renatus Kilongozi. baadaye kadri siku zilivyokuwa zinasonga Nilifahamiana na mgombea ubunge wetu wa chadema ndg Wilfred Lwakatare. kwa kweli wanafunzi kutoka vyuoni tulikiwa wengi lakini kwa sababu hapakuwa na malipo yoyote wengi walikata tamaa na kuondoka kwenye kampeni. mimi niliendelea na ikatokea kuwa na ushawishi mkubwa baada ya kuhutubia mkutano mmojawapo. katika mkutano ule nakumbuka nilikuwa nimeandaa propaganda dhidi ya kagasheki ambayo nilikiwa nikiisoma kwa kiitaliano na kisha kutafsiri kwa kiswahili. ilihusisha pia kashfa dhidi ya kagasheki. propaganda ile ilikuwa na nguvu sana kiasi cha kuifanya redio kasibante inayomilikiwa na kagasheki kutumia masaa mengi kwa siku kunishambulia mimi wakihoji chadema ilikonitoa. ilibidi tuunde propaganda hizo kwa sababu timu ya kampeni yetu haikuweza kupata kashfa yoyote yenye maana dhidi ya kagasheki. nadhani huyu mtu ni kati ya wanasiasa waadilifu katika CCM. ilivyokuwa ilifikia sehemu kwa sababu ya makosa ya huko nyuma mgombea wetu kuna maeneo alikwepa kabisa kwenda kufanya kampeni na mimi kwenda kwa niaba yake. kutokana na hayo hata familia ya ndg Lwakatare walithamini sana mchango wangu wakati huo na kwa kweli niliendelea kuwa rafiki wa familia yao nzima. japo tulipoteza ubunge na kushindwa lakini urafiki wetu ulikuwa umejengeka. Ni wakati huu wa kampeni hizi nilifahamiana na mama Conchesta Rwamlaza mbunge wa viti maalum kagera kupitia chadema. wakati huo akiwa hajakuwa mbunge. nakumbuka wakati mmoja katikati ya kampeni nilipata tatizo lililonilazimu kusafiri dar es salaam. lwakatare akihofia kuwa nilikiwa nimekata tamaa kutokana na kufanya kazi bila malipo aliomba mkutano wanichangie fedha. na kweli zikachangwa fedha japo kwa kweli haikuwa vile. nilisafiri dat na kurudi siku aliyofika dokta slaa bukoba. niliyoa hotuba za awali. tulishindwa kwa haki na baada ya tathmini tulitawanyika na kurejea dar es salaam. Hamis Kagasheki akiwa waziri wa mambo ya ndani aliporejea dar alikuwa ananipigia simu na kuniomba tukutane. niliogopa na kubadili line ambayo nayo aliipata sikuwahi kufahamu alikuwa akiipata namna gani. baada ya muda nikiogopa kashfa nilizokuwa nikiungurumisha dhidi yake kwenye kampeni niliomba vijana wa brigade wanisindikize. tulikwenda wizara ya mambo ya ndani wale vijana wakabana sehemu nikaongea naye kwa dakika kama 45. kwa kweli nilishangaa sana kwamba hakuulizia chochote juu ya mambo ya kampeni bali alisema alitaka kunifahamu na akawa anajadili baadhi ya wabunge wetu wapya na kuwasifia. wakati naondoka alinipatia elfu 40 akisema tugawane umaskini na akiahidi kuwa angeniita tena. mpaka naandika makala haya hajawahi kunitafuta tena. kwa hiyo msomaji aone kuwa nimekuyana na Lwakatare kwenye harkati za chama na kuwa hatuna undugu wowote zaidi kuwa undugu wetu ni chadema. baada ya uchaguzi ule Lwakatare aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa ulinzi na usalama taifa wa chama. kutokana na imani aliyokuwa nayo kule kwenye uchaguzi bukoba: nilifanya kazi bila malipo na mara kadhaa nikikataa kupewa rushwa kutoka kwa wapinzani wetu alipendekeza kwa viongozi wetu wakuu kuwa anaunda kikosi maalum na kwa ajili ya kazi maalum. tangu wakati huo ninafanya kazi katika kikosi hicho. japo kwa sasa naona chain of command haiko moja kwa moja lakini kuna majukumu yangu kadhaa bado nayatimiza. kwa maadili na kanuni za kazi hii haya hayawezi kuandikwa katika makala za magazetini. kwa nafasi yangu nikawa na jukumu la kukusanya yaarifa mbalimbali za ndani ya chama na baadaye hata nje ya chama. moja wapo ilikuwa kuchunguza mienendo ya wabunge wetu majimboni kwao na utendaji kazi wao na kuyafiti juu ya migogoro ndani ya chama. hapo mwaka 2011 wakati wa uchaguzi wa BAVICHA uliomuweka JOHN HECHE madarakani mimi niliingia katika vikao vyote japo sikuwa na uongozi wowote unaofahamika na wengi. mfano katika mkutano wa uchaguzi ilibidi niingie kama mwenyekiti wa wilaya ya bukoba vijijini kwa sababu huyo hakuwa amekuja. jambo baya hapa ni kuwa kuna ofisa mmoja alilipwa fedha za mtu huyu ambaye hakuwepo kwenye mkutano. katika uchaguzi ule ulioghubikwa na mizengwe, kwanza Habib Mchange alienguliwa kwa tuhuma za rushwa. baadaye aliunganisha nguvu na akina Mtela Mwampamba na kundi lote lililokuja kujulikana kama PM7 ama masalia. japo ni kweli mchange alitoa rushwa lakini hata kama asingekutwa na tuhuma hiyo bado kulikuwa na mpango wa kumwengua. Kisha usiku wa kuamkia uchaguzi John Shibuda akiwa anaunga mkono kambi ya akina Ben saanane alikuwa akigawa rushwa hovyo huku akijiiya mzee wa fitna. usiku kucha watu wakitembeza rushwa nami nikiwa nao maeneo mbalimbali, ni mimi niliyeandika ripoti iliyopelekea baadhi ya watu kuondolewa katika uchaguzi ule. nilikabidhi ripoti hiyo mapema siku hiyo asubuhi kwa dokta Slaa na wakati tunajadili yaliyomo alikuja John Mrema pia. mzee Mtei na Marando walikuja baadaye kwa hiyo haeakusikia nilichokiwasilisha ikabidi wapate ushahidi. mimi sasa nisingeweza kutoa ushahidi mbele ya wengi so ikabidi Ephata Nanyaro na Deo Kisandu wakatoe ushahidi. ni bahati mbaya yena kuwa Kisandu naye kaenda CCM. ukumbini hali haikuwa nzuri kwa Heche kwani kampeni ya akina mchange ilikuwa na nguvu. ilibidi nguvu ya ziada itumike kwa kuwatumia wabunge vijana kupiga debe pro Heche. akina sungura na marehemu Regia Mtema walifanya kazi kubwa. baadaye kwa kuhofia malalamiko juu ya kuengua watu wengi tulipendekeza kutengeneza propaganda kuwa walioenguliwa walikuwa wamekamatwa na walinzi wa chama wakiwa na silaha za mapanga eti kushambulia viongozi. dokta Slaa mwenyewe ndiye aliyetoa tangazo hilo. kwa muda wengi wameamini kuwa lilikuwa jambo la kweli wakati kwa kweli tulikuwa tumelipika tu kujaribu kupunguza lawama. sambamba na hayo mgombea Juliana Shonza alikuwa hatakiwi na chama pia. lakini kosa likafanyika aliyekuwa akigombea naye Gwagisa Mwakasendo akatoroka ukumbini na ilipobidi kurudia uchaguzi Shonza akawa yuko peke yake. hatujui ingekuwaje kwa hakika lakini mimi nadhani kama Gwakisa angekuwa ukumbini basi angekuwa makamu mwenyekiti wa BAVICHA. Shonza alitofautiana na mwenyekiti na baraza lake na hatimaye alisimamishwa uanachama na kutimkia CCM. labda tulikuwa tumeona vema juu ya suitability yake. kisha kuondoka DUCE julai 2011 tulikuja kwenda Igunga kwenye uchaguzi mdogo baada ya Rostamu kubwaga manyanga. mimi nikiwa na majukumu maalumu vilevile. uchaguzi ule kwa kumbukumbu yangu ya karibuni ulikiwa wa kufa na kupona. tunajua pamoja na mambo mengine Masoud Mbwana kada wa chadema alikufa na Mussa Tessha alimwagiwa Tindikali. Vyama vya CCM na CHADEMA vimekuwa vinatupiana lawama juu ya matukio haya. je kuna anayejua ukweli wa matukio hayo? Tuendelee wiki ijayo.
.... Ludovick 0757 314961
--Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACMr6QisAiehTtQqGLAs1GrnLtmz-V_1NtZ_GWiiE7Co01LAPg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments