Wadau,
Kwa kuwa kumekuwepo na kambi mbili katika suala hili la katiba mpya ya nchi yetu, na kwa kuwa maridhiano ni jambo ambalo haliepukiki katika kuipata katiba mpya ya nchi yetu kwa sasa, napendekeza viongozi wa kambi hizi mbili sasa wajitokeze hadharani, kama alivyofanya Mzee Warioba na timu yake, kutueleza watanzania ni nini hasa wanachokiamini katika suala hili la katiba mpya ili sisi wananchi tuamue njia itakayotufikisha salama huko tuendako.
Ili kulifanikisha hilo, napendekeza sasa kwa wadau wa habari kuandaa midahalo miwili, ikibidi yenye awamu mbili kwa kila mdahalo ili kutoa fursa nzuri kwa washiriki kutueleza kile wanachokiamini na pia kukubaliana way forward. Nafikiri midahalo hii, kama itaandaliwa vizuri, inaweza kulizuia taifa kuingia kwenye mipasuko na gharama zisizokuwa za msingi endapo itazaa moyo wa maelewano na hatimaye maridhiano. Maridhiano hayo yanaweza kutoa nafasi ya kutafuta nafasi ya kurekebisha kasoro kubwa zilizomo kwenye katiba pendekezwa na hivyo kuipatia nchi katiba mpya itakayotufaa watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yetu kama ambavyo amependekeza Mzee Warioba kwenye mdahalo wa jana pale kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Napendekeza mdahalo wa kwanza uwe ni kati ya iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba (ambapo anaweza kuwepo Mzee Joseph Sinde Warioba, Humphrey Polepole na mjumbe mmoja kutoka Zanzibar) na Uongozi wa BMK (ambapo anaweza kuwepo Samwel Sitta, Ameir Pandu Kificho na Andrew Chenge). Mdahalo wa pili uwe kati ya UKAWA (napendekeza awepo Maalim Seif Sharif Hamad, Tundu Lissu na Mbatia) na Tanzania Kwanza (Hamad Rashid, Stephen Wasira na Anne Makinda). Idadi ya wajumbe hawa inaweza kuongezeka ama kupungua, na pia kubadilika kutokana na utayari pamoja na mahitaji.
Midahalo hii inaweza kurushwa na vituo vyote vya TV na Redio, na igharamikiwe na serikali kama njia mahususi ya kuwasaidia wananchi kuelewa ni nini hasa kinachobishaniwa, na pia kupata fursa za kupiga simu kuuliza maswali, kushauri na pia kutoa mapendekezo yao, ikiwa ni pamoja na ushiriki wa moja kwa moja ukumbini. Pia itokeapo consensus, ni rahisi wananchi kujua imepatikanaje na hivyo kujenga umoja wa kitaifa na kuaminiana, jambo ambalo ni muhimu katika zoezi hili muhimu kwa taifa letu kwa sasa.
Kwa hayo machache, naomba kutoa hoja.
SA.
--Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAPPZ%3DWzBgqxDzhNNAhTd-8st63UVEy8mUTO_BTod9oUnffCs0A%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments