[Mabadiliko] ANGALIZO: Daftari la Kuandikisha Wapiga Kura Uchaguzi Serikali za Mitaa Balaa!

Thursday, November 27, 2014
Wananji,

Nipo huku vijijini kufuatilia kinachoendelea katika matayarisho ya mwisho kuelekea uchaguzi serikali za mitaa.

Katika pitapita zangu za kukagua, nimegundua kasoro moja ambayo huenda imeandaliwa ki-mkakati na serikali ya CCM ili kuja kuwaliza wapinzani kwenye uchaguzi huu.

Kile kitabu kinachotumika kuoroshesha majina ya wapiga kura kwenye vituo vya kujiandikisha kina karatasi zenye sehemu ua kuorodhesha majina ya wapiga kura 16 kila page (yaani 1-16) lakini hazina serial number za page yaani page 1,2,3,4,...hadi ya mwisho wa kitabu.

Page zote zinazotumika zinafanana na hata ikitokea page moja ikachanwa na kutupwa wakati wa kubandika majina kwemye vitu vya kupigia kura, hakuna namna ya kujua maana hutajua ni page ipi inakosekana!

Nimewahoji wasimamizi huku vijijini nao hawajui lolote zaidi ya kuseama wao wamepokea kila kitu kama kilivyo na hawana la kufanya.

KWA UZOEFU WANGU:
CCM watatumia upungufu huu kupoteza kurasa zilizoandikwa majina mengi wanayoona ni ya wapinzani ili kuwazuia wasipige kura kwa kuaambiwa majina yao hayapo kwenye kituo husika.

SOLUTION:
Viongozi au wawakilishi wa vyama vya upinzani waende kwenye kila kituo na kuomba kuhesabu kurasa za kitabu kizima ili kugundua vitabu vinavyotumika vina jumla ya kurasa ngapi, ili ikitokea kasoro, warejee kwenye kitabu na kuhesabu idadi ya kurasa ili kuona kama zilizobandikwa na zilizobaki kwenye kitabu zinaleta idadi kamili ya kurasa za kitabu kizima.

AU
Wapinzani watumie mawakala wao kuchukua orodha ya majina yote iliyomo kwenye daftari linalotumika na kuiingiza kwenye daftari tofauti ili siku ya siku kukikosekana jina wajue lilikuwa la nani na alijiandisha wapi na tarehe ngapi.

Just play my part..... play yours!

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CADVpsxSv-Kmgu2SLMHFe2UpvHeGvsvBhqtxg3v6Wcmi2wsobzQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments