Ndugu zangu,
Wasadikika hawaishiwi maajabu. Ngoma Kuu ya Sakata la Eskroo imehitimishwa leo. Tayari yametolewa mapendekezo, kuwa Uwanja Mkuu wa Ndege kwenye nchi ya Kusadikika uitwe ' Dar es Kroo International Airport' . Ni kwa kuwa Dunia sasa inaifahamu zaidi nchi ya Wasadikika kwa Sakata la Eskroo!
Na ajabu ya Wabunge wa Nchi ya Kusadikika ni ukweli kuwa, siku ile Profesa wao aliyebobea katika masuala ya miamba na madini, na hata amejulikana ulimwenguni kote, aliposema, kuwa mmoja wa Wabunge wa Nchi ya Kusadikika, Wole Soyindeka, kimsingi alifeli Form Four na hivyo hakuwa na akili ya kumkosoa Profesa. Na Profesa alikuwa tayari kutoa CD kwa Wabunge kuangalia na kutafakari kama Mbunge huyo anastahili kuwa mwanachama kwenye chama kikuu cha nchi ya Wasadikika. Wabunge Wasadikika walimshangilia sana Profesa wao.
Ajabu ni juzi hapa, kwenye Bunge hilo hilo. Mbunge aliyefeli Form Four, Wole Soyendika, alisimama na kumwambia Profesa wa Miamba kuwa hana lolote isipokuwa ni dalali wa Mafisadi. Wabunge Wasadikika walimshangilia sana Mbunge mwenzao aliyesemwa na Profesa kuwa alifeli Form Four!
Naam, kwenye Nchi ya Kusadika wanaamini pia, kuwa anayecheka mwisho ndiye aliyefaidi utamu wa kucheka!
Maggid ,
Msamvu, Kitongoji kwenye Nchi ya Kusadikika.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye4FfZEkWjr5ycWQJSR%2Bpy%3DGNC6-9pCUYhb5B%2BNnPBOUNw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments