[wanabidii] WALIOKUWA WAJUMBE WA TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA WAKAE KIMYA

Wednesday, October 22, 2014

HUYU POLE POLE ANATUONA SISI WATANZANIA WAJINGA.

NAWASHAURI WALIOKUWA WAJUMBE WA TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA WAKAE KIMYA.

Kitendo cha wajumbe wa kamati ya kukusanya maoni ya katiba mpya kuendelea kupiga kelele na kampeni ya kuwashawishi wananchi kuikataa rasimu pendekezwa kunatia shaka kidogo.

Hivi hawa wajumbe walikuwa hawajui kuwa mchakato wa katiba mpya una hatua kuu tatu yaani ukusanyaji wa maoni kazi iliyofanywa na Tume, Kujadili maoni kazi ya BMK na kura ya maoni ambayo sis wananchi tunahusika.

Kila hatua kati ya hatua hizo upo kisheria kabisa sasa kitendo cha hawa wajumbe kuendelea ku defend rasimu yao waliyoandika na kuikataa hii pendekezwa kuna maanisha kuwa kulikuwa hakuna haja ya BMK. Kulikuwa na haja gani ya kuwa na BMK kama maoni yaliyokusanywa hayatachambuliwa na kuboreshwa aidha kwa kuondoa baadhi ya mambo au kuyaongeza??

Kwa nini hawa wajumbe wa tume ya maoni haituachii muda wa kusoma rasimu hii pendekezwa na kuamua sisi wenyewe?? huyu Humphrey Polepole ni kwanini anatusaidia kuisoma rasimu pendekezwa na kutushauri tupige kura ya hapana?? anatuchukuliaje labda sisi watanzania:-

1. Kuwa hatujui kusoma 
2.Kuwa hatujui kufanaya uchambuzi wa mambo
3. Ni wajinga sana
4. Yeye ndiye anayejua kila kitu hapa Tanzania

Kwa nini usikae kimya kama kina KABUDI ili tuisome kwanza tuimalize hii rasimu halafu ndio tuingie kwenye mijadala?? kwa nini unatusomea??

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments