[wanabidii] Ulinzi wakati wa makabidhiano ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa

Wednesday, October 08, 2014
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi David Misime ameeleza kuwa kutokana na tukio la kihistoria ambalo litafanyika tarehe 08.10.2014 ambapo Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mh. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar watakabidhiwa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mkoa wa Dodoma hususani Dodoma Mjini.

Ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi umeimarishwa zaidi, doria za miguu, magari, pikipiki na mbwa na farasi nazo zimeimarishwa. Pia vyombo vyote vya dola tumeimarisha zaidi ushirikiano hasa kubadilishana taarifa mbalimbali na wote mitaani kufuatilia tukio hili muhimu kwa kutumia mbinu zote walizo nazo.

Niwahakikishie wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wageni wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa tunachowaomba ni ushirikiano wao pale watakapomtilia mashaka mtu yeyote au jambo lolote wajulishe Polisi haraka nao watalifanyia kazi. Pia wenye nyumba za kulala wageni waimarishe ulinzi kwenye maeneo yao ya biashara na kuwapa maelekezo sahihi wafanyakazi wao na wakitilia shaka mgeni yeyote watoe taarifa polisi.

Pia wananchi wote pamoja na wageni wote watii sheria bila shuruti na yeyote anayepanga kukiuka sheria ili kuvunja amani na utulivu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa mamlaka waliyopewa Jeshi la Polisi.

Taarifa hii imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments