Ndugu wadau,
Kwa sasa nipo Dar es Salaam kwa wiki mbili tatu hivi. Ni vyema kama itawezekana kuonana na wadau ambao wanapenda kutafuta udhamini wa elimu ya juu ughaibuni na kupeana scholarship seminar. Kama kuna watu ambao wanaweza kurahisisha suala hili itakuwa vyema mno.
Lengo la seminar ni kupeana utaratibu, mbinu na uzoefu wa utafutaji udhamini wa elimu ya juu. Kikubwa nachopambana nacho ni sehemu ya kufanyia seminar ya kuwasaidia wadau.
Kwa wale ambao wa waalimu, iwe ni sekondari au vyuo, tunaweza kufanya arrangement na nikawa guest speaker kwa wanafunzi wa darasa lako. Hii itasaidia wanafunzi kujua hatua mbalimbali na nini mbeleni.
Huduma hii ni BURE 100% kama nifanyavyo kila siku.
Kwa mwenye connection za kwenye TV na Radio nitafurahi kama nikiweza kuongea huko. Mwaka 2009 na 2010 niliongea kwenye TBC Radio, TBC TV, na ITV. Iliweza kusaidia wengi kuwafumbua. Nipo naongea na baadhi ya wadau ila kuna usumbufu mtu kukupa airtime. Kukosa kuongea kwenye vyombo hivi vya habari nitakuwa nimewanyima fursa watanzania wengi kupata udhamini nje.
Namba yangu ya simu ni 0768 393055.
Ernest Makulilo
Scholarship Winner (over $120,000 scholarship money)
Scholarship Blogger MAKULILO SCHOLARSHIP BLOG
0 Comments