[wanabidii] Taarifa ya SUMATRA ya utaratibu wa daladala zilizohamishiwa Mawasiliano Towers

Monday, October 20, 2014

KUHAMISHIA DALADALA KITUO CHA SIMU 2000
(NYUMA YA MAWASILIANO TOWERS) KUANZIA ALHAMIS TAREHE 23.10.2014


Baada ya kituo cha Simu 2000 kukamilika SUMATRA kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni na Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Kinondoni tumekubaliana kufungua kituo hiki tarehe 23.10.2014 asubuhi kwa daladala ambazo zilikuwa zinaishia au kuanza safari katika kituo cha daladala Ubungo.

Kila dereva anatakiwa kufuata utaratibu ulioelekezwa hapa chini ili kuondoa usumbufu usio na tija.

1. DALADALA ZINAZOTOKA MASAKI
zikifika barabara ya Shekilango zitaingia kulia kwa kutumia barabara ya TANESCO inayokwenda moja kwa moja kituoni simu 2000 na zitarudi barabara ya Shekilango kwa kutumia njia hiyo hiyo ya TANESCO.

2. DALADALA ZINAZOTOKA KARIAKOO, POSTA na KIVUKONI
zikifika mataa ya Ubungo zitaingia kulia (barabara ya Sam Nujoma) kwenda kituoni Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo

3. DALADALA ZINAZOTOKEA BARABARA YA MANDELA
zitavuka mataa ya Ubungo (kwa kutumia barabara ya Sam Nujuma) na kwenda kituoni Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo.

4. DALADALA ZINAZOTOKEA MWENGE
zikikaribia jengo la Mawasiliano Towers zitachepukia kushoto kwa kutumia service road inayopita mbele ya Mawasiliano Towers hadi kituoni simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara ya Sam Nujoma (sio servive road).

5. DALADALA ZINAZOTOKEA KIMARA NA MBEZI
zikifika mataa ya Ubungo zitaingia kulia kwenda kituoni simu 2000. zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo.

Conrad Shio
Afisa Mfawidhi SUMATRA –DSM
0755 660 016

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments