[wanabidii] Taarifa ya kiwanda cha A to Z kuhusu mfanyakazi aliyefia kazini

Sunday, October 19, 2014
TAARIFA KW A VYOMBO VYA HABARI

Tarehe 13/10/2014 siku ya Jumatatu majira ya saas moja asubuhi ilitokea ajali katika moja ya viwanda vyetu. Kwa bahati mbaya nati kubwa inayoshililia mfuniiko wa mashine ya kufungia marobota ilikatika na mfuniko huo kudondoka chini. Bahati mbaya pale chini karibu na hiyo mashine alikwepo mfanyakazi akifanya kazi. Alidondokewa na kuumia kichwani. Meneja wa idara alifanya haraka kumpeleka hospitlai kwa matibabu.

Taratibu za kujaza fomu ya ajali kwa mujibu wa sheria ya OSHA na kuwaita maafisa wa OSHA zilifanyika haraka. Maofisa wawili toka OSHA walifika kiwandani kukagua eneo la tukio.


Hospitali daktari alimchunguza mfanyakazi huyo aliyeumia akaagiza apelekwe chumba cha wagonjwa mahututi. Kwa bahati mbaya mfanyakazi huyo mwenzetu alifariki dunia majira ya saa nne na nusu asubuhi hiyo hiyo.

Baada ya kupata taarifa za msiba toka hospitalini uongozi wa kiwanda uliwasiliana na ndugu wa marehemu ambao walikuja kiwandani kwa majadiliano ya namna ya kumhifadhi mwenzetu aliyetangulia mbele za haki.

Tuliwaeleza ndugu wa marehemu mpiango yetu ambapo tuligharamia mazishi kwa kununua sanduku, sanda, na manukato pamoja na kutoa usafiri wa kuupeleka mwili wa marehemu kijijini kwao kwa mazishi. Pia kiwanda kimetoa pesa taslimu zikiwa ni rambirambi kwa wazazi wa marehemu. Msafsara wa mazishi umeambatana na Charls Magimbi kwa niaba ya uongozi wa kampuni.

Jambo la kushangaza ni kuwa kuna taarifa zisizo sahihi na za kupotosha zinazotolewa na watu kuhusu ajlai hii. Tunachukua furasa hii kuwajulisha umma kuwa kilichotokea ni ajali ambayo haizuiliki na sio upotofu unaotolew ana watu ili kuharibu jina na heshima ya kiwanda chetu.

Kiwanda chetu kina cheti cha ISO tangu 2011, kila mara wakaguzi wa kimataifa wanakuja hapa kukagua vigezo na vitendea kazi li kukidhi mahitaji ya kimataifa.

Tunawashukuru sana viongozi mbalimbali wa Serikali yetu wateja wote ambao wamekuwa wanatuandikia mezeji za pole katika wakati huu mgumu kwetu.

Mazishi yanafanyika saa kumi leo hii. Muda huo (saa kumi jioni ) Mkurugenzi wa Uzalishaji wa idara iliyotokea ajali watasimamisha kazi kwa muda wa dakika mbili kutoa heshima kwa mwenzetu aliyetangulia mbele za haki.

MWENYEZI MUNGU AILAZE MAHALI PEMA ROHO YAKE PEPONI.

AMINA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments