Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA KUU Kanda ya Dar es Salaam Jana ilibariki mwenendo wa Bunge la Katiba kuwa liliendeshwa kulingana na mamlaka yake kisheria.
Pia Mahakama hiyo imesema kuwa Bunge hilo halikuwa likifungwa na Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwa Bunge hilo ndilo lenye mamlaka ya kutunga Katiba mpya na si Tume.
Mahakama Kuu ilitoa msimamo huo jana wakati ikitoa sababu za uamuzi wake katika kesi ya mamlaka ya Bunge la Katiba iliyofunguliwa na Saed Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kubenea aliwakilishwa na wakili Peter Kibatala.
Hata hivyo, Kubenea ameanza mchakato wa kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi huo na tayari ameshawasilisha taarifa ya kusudio hilo.
Katika kesi hiyo Namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea alikuwa akiiomba mahakama hiyo itoe tafsiri ya Mamlaka ya Bunge la Katiba kwa kuzingatia Kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.
Pia aliiomba Mahakama itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na mamlaka hayo ni ya kiwango gani.
Katika uamuzi wake uliotolewa Septemba 25, Mahakama Kuu ilisema kuwa haina mamlaka ya kuliwekea mipaka Bunge la Katiba kuhusu asili na kiwango cha marekebisho au maboresho ya Rasimu ya Katiba.
Uamuzi huo ulisomwa na kiongozi wa jopo la majaji watatu waliosikiliza kesi hiyo, Jaji Augustine Mwarija kwa niaba ya wenzake, Dk Fauz Twaib na Aloysius Mujulizi.
Jopo hilo pia lilisema kuwa kulikuwa na utata wa kimaana katika kifungu cha 25, katika matoleo mawili ya sheria hiyo, yaani toleo la Kiswahili na toleo la Kiingereza.
Hata hivyo, Mahakama ilitoa amri hizo kulingana na uharaka wa kesi hiyo, bila kutoa sababu za uamuzi huo na badala yake ikapanga kutoa sababu hizo jana.
Wakati ikitoa sababu za uamuzi wake jana, Mahakama Kuu ilisema haishawishiki kuwa Bunge la Katiba lilikuwa linafungwa na Rasimu ya Tume kwa kufuata kila masharti ya Rasimu hiyo yawe ni ya msingi au la.
Akisoma kwa niaba ya jopo hilo, Jaji Dk Twaib alisema kwa maoni yao kuwa kuna baadhi ya miundo ya msingi katika rasimu hiyo, Bunge la Katiba halikuwa na mamlaka ya kuyabadili, hayaungwi mkono na sheria.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi, Oktoba 8 Mwaka 2014.
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments