Pichani ni Zuhura Matata mgonjwa mwenye uhitaji wa upasuaji utakaofanyika nchini India.
Kipindi cha "Mimi na Tanzania" kinachoongozwa na mrembo aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu, kinatoa shukrani kwa watanzania wote walioguswa na kufanikisha michango ya matibabu ya Zuhura Matata mwenye tatizo la kuvimba mguu ambao unahitaji Oparesheni nchini India.
Kupitia Akaunti yake ya mtandao wa kijamii Facebook muongozaji wa kipindi hicho Hoyce Temu ameandikia ujumbe wa kuwashukuru watanzania. Soma hapa chini.
Zuhura Matata ambaye tulimuombea msaada wa kwenda India kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania, amefanikiwa kupata pesa zote shilingi milioni 15 sawa na dola elfu kumi. Ataondoka tarehe 21 Oktoba kuelekea India na kuanza Matibabu! Usikose kutazama kipindi cha Mimi na Tanzania, Jumapili, Chanel Ten kuanzia saa tatu na nusu usiku. Mimi Hoyce Temu natangaza rasmi kufunga michango kuanzia sasa kwani pesa tulizoomba tumepata zote! Asanteni Tanzania!
Pichani ni Mtangazaji wa Kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu alipomtembelea Zuhura Matata kwa ajili ya mahojiano.
Zainul A. Mzige,
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments