KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI BORA KULIKO YA SASA, HONGERA MH. RAISI, HONGERA WATANZANIA.
Katika historia ya uandishi wa katiba mpya duniani hakuna nchi yeyote ambayo iliwahi kuandika katiba mpya ikakidhi matakwa ya wananchi wote na taifa kwa 100%. Katiba si msaafu wala si biblia kwamba haiwezi kufanyiwa maboresho. Leo hii jambo ambalo tumeliona lina tija na manufaa kwa taifa na tukaliingiza kwenye katiba, kesho tutaliona halina tija na tutakubaliana kuliondoa au kuliboresha. Vilevile jambo ambalo leo tumeliona halina tija na kutoliingiza ndani ya katiba kesho tutaona umuhimu wake na tutakubaliana kuliingiza ndani ya katiba yetu.
Katiba inayopendekezwa imetambua haki za makundi mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wasanii, vijana, wanawake na wengine. Pia katiba inayopendekezwa imetambua haki bunifu, mgombea, binafsi, maboresho katika muungano wetu sambamba na kuweka mfumo bora wa kusimamia rasirimali za taifa na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya rasirimali. Kundi pekee ambalo linadhani halijatendewa haki katika katiba hii ni kundi la wanasiasa wachache ambao kwao tafsiri ya katiba bora ni ile inayokidhi maslahi yao ya kisiasa. Hili ni jambo ambalo watanzania hawana budi kulikataa.
Jambo la msingi ambalo kila mtanzania anapaswa kukubali ni kwamba katiba inayopendekezwa ni bora kuliko ile ya sasa. Wakati ambapo baadhi ya watu wakiipinga na kudai kwamba haiwezi kulivusha taifa letu, wapo watanzania tena asilimia kubwa ambao wanaiona katiba inayopendekezwa kuwa ni chombo madhubuti ambacho kitachochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja, na ikifika wakati watanzania wote tukawa na mawazo yanayofanana basi tujue kwamba tunapaswa kujitazama upya. Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida na
hiyo ndiyo afya ya demokrasia iache ichukue nafasi yake. Tupingane kwa hoja bila kuhatarisha amani ya taifa letu.
Hongera Mh. Raisi Dr. Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa uliyoifanya. Hili ni jambo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Taifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Taifa letu kuandika katiba yake kwa kushirikisha wananchi wake. Yapo mataifa ambayo yaliwahi kuandika katiba zao kwa kutumia Bunge la katiba pekee, wapo waliogeuza Bunge la kawaida na kuwa Bunge la katiba. Kwa taifa letu, mchakato umekuwa wa kidemokrasia zaidi kiasi kwamba wapo wanazuoni, wanasiasa na mataifa mbalimbali ambao wameishangaa Tanzania kwa kuruhusu demokrasia kwa kiwango hiki. Kwa hakika Mh. Rais anastahili pongezi na daima watanzania tutakukumbuka na jina lako haliwezi kufutika katika fikra zao.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments