[wanabidii] JE UPO SALAMA ? WAWEZA KUJIFUNZA PENGINE HAPA KIDOGO.

Monday, October 06, 2014

Leo asubuhi nimefika ofisini. Nilikuwa najiandaa kwenda mkutanoni. Nimefika kama saa moja na nusu hivi.`

KILICHOTOKEA.
Mara akaingia mzee mmoja...Kajitambulisha (nipo ofisini kwangu-nakuwa peke yangu). Akasema anatokea Manzese SDA church, akasema ananifahamu, akasema ananifahamu hata nikiwa UDSM, akasema hata nilikuwa kiongozi wa wanafunzi pale.akasema amekuja kwangu anaomba nimsaidie mwanae amepata Div 2 form six ameomba vyuo amekosa. Akasema wameambiwa waombe tena, fani anayotaka yeye haipo kwenye kuomba tena. Anataka asomee Mafuta na Gesi. Aksema jambo la pili,ana mzigo mkubwa wa kusomesha watoto, wa kwake 6 na wa mdogo wake 7, jumla wapo 13. Akasema kwa bahati mbaya mke wake alifariki miaka 10 iliyopita.

NILIVYOMJIBU,
Moja, nikasema mtoto wake ndiye anaweza kuwa anajua zaidi kwa nini amekosa nafasi. Pengine fani alizoomba hakufikia kiwango kinachotakiwa kwenye fani hizo. Ansema, hataki kwenda kusomea ualimu na fani ambazo hakutaka.

NIKAMWAMBIA, sasa hawezi kuchagua fani, kwa nchi yetu unalazimika kusoma kitu pengine kutokana na matokeo yako,sio unachopenda. nikamwambia, kusomea kitu haimaanishi lazima uje kufanya kazi za fani hiyo maishani. Lakini nikwamwambia kwa fani alizoomba, aone kama kuna mtu kachukuliwa mwenye matokeo pungufu kuliko yako,au sawa na yeye akate rufaa.

TATIZO LANGU.
1. Mtu kaja ofisini kajitambulisha yeye, anaonyesha kunifahamu(katoa taarifa za kweli)....Lakini anachosema, yeye ni mtu mzima, inaonyesha ameambiwa..HASEMI amenifahamu vipi.
2. Tatizo la pili, ulinzi kwenye ofisi nyingi si salama. Mtu anatakiwa akiwa kwa walinzi, wamuulize anashida na nani? halafu wachukue maelezo yake, pasipo kusema mtu yupo ndani au la....wamwambie mtu wa ndani, ndiye aseme mtu aingie au hapana(hii ifanyike getini kwa mlinzi)/...............JE OFISI YAKO INAFANYA HAYO.

FUNZO.
Kila siku tunajifunza....Kuna wakati nilifunza kwamba kwa mfano wanasiasa, mkiwa sehemu, Ukienda pembeni midogo/pengine kujisaidia(.....haja ndogo/kubwa)...kama ulikuwa unakunywa Juice,au Soda,au Maji wenzetu wa moja baridi moja moto, ukirudi tu...USIENDELEE NA KINYWAJI CHAKO huwezi jua nani kaweka nini.

Yule mzee ni mtu mzima, baadae nikapiga moyo kondo, nikauliza vitu tumewahi onana wapi?...ama hakusikia vizuri swali ama ameruka........basi akajibu...Ahaaaaaaa sijapita popote nimekuja kwako tu kukuomba msaada.

Pamoja na mengine nikampa namba ya kiongozi wa TAHLISO mmojawapo ili kama mwanae ataona ameonewa, akihitaji ushauri zaidi aende huko.

MWISHO.........Ukienda kwa mtu, ni vema kusema nani amekutuma, inaondoa maswali mengi. Kama kuna mtu amempa taarifa zangu, basi ni vema angemsema yeye, au huyo mtu angeniambia mimi kuwa kuna mtu atakuja ofisini kwako,ana shida fulani.......

TUNAANDIKA YANAYOTOKEA ili wote tujifunze , wote tupo safarini...kila siku tunasikia mtu 'ameumizwa nk' mazingira ni muhimu tukajirekebisha......

Nimeongea na walinzi wetu, WAMEPOKEA USHAURI

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments