Abood Jumbe hali tete, alazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
RAIS mstaafu wa awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abood Jumbe Mwinyi (94), yupo hoi baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na maradhi ya moyo. Akizungumza Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Muhimbili, Doris Ishenga,alisema Jumbe alipokewa hospitalini hapo tangu Oktoba 12, mwaka huu. Amelazwa katika Taasisi ya Moyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. Alisema kwa mujibu wa taarifa za madaktari za Kitengo cha Moyo hospitalini hapo, baada ya kumfanyia uchunguzi wamebaini Jumbe anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo hali inayobabishwa na kuwa na umri mkubwa. "Ni kweli Alhaj Jumbe alifikishwa hapa Muhimbili tangu Jumamosi iliyopita na amelazwa katika wodi ya moyo akisumbuliwa na maradhi ya moyo. "Unajua ugonjwa huu unawapata zaidi watu wenye umri mkubwa, madaktari wamesema hali yake si mbaya na wala si nzuri sana," alisema. Jumbe alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 hadi 1984 akishika nafasi hiyo baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, marehemu Abeid Aman Karume Septemba 5, 1972. Alijiuzulu mwaka 1984 baada ya kutokea mfarakano wa kisiasa kati yake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kile kinachoelezwa kuwa na msimamo wakutaka mfumo wa Serikali tatu ili Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili. Baada ya kutoa msimamo huo, Jumbe alipata upinzani ndani ya Serikali na chama chake na kutakiwa ajiuzulu urais wa Zanzibar. Baada ya uamuzi kutolewa kwenye vikao vya juu vya CCM, Jumbe aliachia nafasi hiyo ambayo ilichukuliwa na Ali Hassan Mwinyi mwaka 1984, ambaye baada ya mwaka mmoja alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments