[wanabidii] WASIWASI WANGU KWA PROFESA SAFARI

Saturday, September 06, 2014

WASIWASI WANGU KWA PROFESA SAFARI.

Akiwa mjumbe wa kamati kuu CHADEMA mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti Tanzania Bara CHADEMA Profesa safari ananipa wasiwasi kutokana na makala yake yenye dalili zote na viashiria vya UDINI,nini wasiwasi wangu;

1. Akisisitiza hoja yake huku akionekana ni mwenyekumuunga mkono Zitto Kabwe anasema yeye ni mwanaharakati na amepania kuondoa hisia za UDINI na UKANDA zilizokithiri ndani ya chadema akidai CHADEMA kunamazingira ya UKRISTO huku CUF kukiwa na viashilia vya UISLAMU hivyo anataka uongozi ili apambane na udini,kiongozi bora hapaswi kujinadi kwa kujielekeza katika kundi au mlengo fulani.

2. Profesa Safari alienda mbali zaidi kwa kushutumu serikali ya CCM kwa kuwa imewakandamiza waislamu kwa muda mrefu kwa kuwanyima elimu. Nakumbuka mwl Nyerere alitaifisha shule za MISSION zilizokuwa chini ya KATOLIKI kwa lengo la kuwezesha makundi yote kupata elimu bora,leo Profesa Safari anasema waislamu walinyimwa elimu.

Naoenda kunukuu maneno ya Baba wa taifa nitamnukuu "UKIONA MTU ANATUMIA MGONGO WA DINI,KABIRA au RANGI HUYO HAFAI KUWA KIONGOZI" Sina imani na Profesa Safari.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments