Mdogo wangu Happy Katabazi,
Napenda nichukue fursa hii kukupongeza kwa jitihada unazozifanya kama mwandishi, mchambuzi wa mambo ya kisiasa na kijamii. kwa mbali naona maono yako ni kuwa mwandishi mahili, hasa kwa mambo ya kisheria. Pia kwa kusoma makala zako naona unataka uwe mkosoaji wa wale wanaokosoa mfumo wa utawala tulionao sasa.
Happy mdogo wangu baada ya pongezi naomba nikupe ushauri kuwa makala zako zinaonyesha wazi hujaelimika licha ya kuhitimu shahada ya sharia na kuandika habari za mahakamani kwa siku nyingi. Makala zako zinaonyesha unatawaliwa na HISIA na si uharisia. Mbaya zaidi unaonyesha uelewa mdogo wa kile unachokisema!!
Mfano ni makala iliyobeba kichwa cha habari kilichohapo juu. Nani alikwambia anayeandamana ni wakala wa shetani??? na elimu yako ya sharia hujui kuwa duniani kuandamana kudai haki au kupiga lile lisilokubarika ni haki ya binadamu?
Unataka wale wasio na wakuwasemea awasemee nani??
Hivi unajua hawa walioitisha maandamano nchi nzima wanafanya hivyo kwa sababu gani?? Inaonesha wewe ni kipofu na kiziwi kwa kile kinachoendelea Dodoma katika BMK. unaambiwa mabilioni ya hela yatokanayo na kodi ya walala hoi yanateketea bure maana katiba bora haitapatikana... unaziba masikio unawatukana wanaoona mbali zaidi. Hata Mheshimiwa Mwigulu aliliona, wewe unashindwaje kuona?? Mimi siyo mwanasiasa lakini anachokifanya Sita na timu yake ni ubabe!!! nilitegemea mwandishi mahili ulione hilo. basi kama hulioni nyamaza usitukane watu!!!
Hivi unajua ni watoto wa wakulima wangapi wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu wamekosa mikopo huku mabilioni yakiteketea Dodoma?
Unajua ni shule ngapi zenye madawati ya kutosha hapa Tanzania?
Unajua ni sekondari ngapi zenye vyumba vya kutosha wanafunzi wanaochaguliwa na kujiunga na sekondari hizo?
Unajua ni wanachuo wa kike wangapi wanaolazimika kuuza miili yao ili wapate pesa ya kujikimu kwa sababu ya kucheleweshewa pesa za kujikimu na bodi ya mikopo?
unajua ni akinamama wangapi wanakufa kwa kukosa huduma bora ya matibabu (hasa mahali salama na karibu pa kujifungulia)?
Sasa mwanasiasa anaguswa na hali hiyo nahamasisha watu waandamane kupinga kuteketea kwa mabillioni, ili kilichobaki kielekezwe kwenye huduma za jamii.. unamuita wakala wa shetani!!!
Angalia wasomaji wako wasije kukugeuzia kibao wakakuita wewe Happy wakala wa shetani!!!
Jambo jingine, hivi katika katiba ya nchi yetu shetani ni nani? Bora mambo ya shetani na Mungu yaachie wale waliopewa mamlaka ya kumjua nani ni shetani na nani ni Mungu. la sivyo hata mheshimiwa rais wako utamuita shetani, askofu anayepinga kinachoendelea Dodoma utamuita shetani, na wale wote wasioridhika na mwenedo wa BMK utawaita shetani!!!
Ila mungu wako unayemtaja katika makala hii si Mungu wetu tunaomuamini, Mungu wetu huanza na herufi kubwa. kwa hili sitakukosoa sana. na uliyemuita nabii nashawishika kusema ni nabii wa hyuyo mungu wako na si wa Mungu wa waliowengi.
Umeongelea mamlaka. hivi kweli na elimu yako ya sharia unaamini kila kinachoitwa mamlaka kinafanya kazi ya Mungu?? Basi kwa taarifa yako Polisi kazi yao kubwa ni kulinda raia wake na si kuwapiga rai, kuwanyang'anya zana zao za kazi n.k!
Katika Makala yako ya nyuma ulidai wewe ni mwanafunzi wa Hayati Dr. Mvungi. Nina wasiwasi kama ulikuwa mwanafunzi mzuri!!! Makala yako hayaakisi alichokifundisha na kukiamini Dr. Mvungi. wanafunzi wake wataandamana kudai unyang'anywe hiyo degree!!!!
Umeandika shetani peke yake ndiye anapenda mabo ya vurugu!! hivi nini maana ya vurugu?? Hivi uliwahi kusoma katika bibria pale Yesu alipopindua meza na kuwatimua wafanya biashara katika hekalu?? Alichokifanya Yesu ndo unaowaita shetani wanatamani kukifanya pale Dodoma.. sasa utasema Yesu alisababisha vurugu hivyo naye ni shetani??? akina Sita wamepoteza uhalali wa kuwa pale mjengoni.
Happy unajichanganya... juzi Polisi walisababisha vurugu wakapiga waandishi wa habari na kuwajeruhi. sasa nao ni mashetani?
Mwisho lugha na uwasirishaji wako havioneshi una elimu ya chuo kikuu... mwandishi aliyemaliza kidato cha nne na akapitia kozi ya miezi mitatu ya uandishi anaweza kuwasirisha makala yake kwa lugha fasaha kuliko wewe.
Kama unataka kuwa mwandishi mahili na mkosoaji epuka kutawaliwa na hisia, chuki na jiendeleze kielimu!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments