[wanabidii] UENYEKITI BAVICHA: PASCAL PATOBASS... NYUMA YA PAZIA NA UFADHILI WA ANTHONY DIALLO.

Tuesday, September 09, 2014

Utangulizi.
1. Pachal Patrobas ni mwajiriwa wa kampuni ya sahara media Group Limited akiwa kama Mwanasheria wa Sahara Media Media Group Limited, lakini pia akiwa kama kwenye kitengo cha HR ya kampuni hiyo. Kampuni ya Sahara Media Group Limited inamiliki vituo vya utangazaji vya Star Tv, Redio Free Africa (RFA) na Kiss FM, inayomilikiwa na Dr. Anthony Mwandu Diallo ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza. Kampuni ya Sahara Media Group Limited ilikuwa ni tokeo la kampuni ya DM Investment Company ambayo iliasisiwa na baadhi ya watu akiwemo Dr. Anthony Mwandu Diallo ambayo kwa mwaka 1992 ilikuwa na mapato ya USD 2.2 millioni na kuwa miongoni mwa kampuni tatu kwa kujiingizia kipato kikubwa. 
2. October, 15 2012 wakati Dr. Anthony Mwandu Diallo anakuwa Mwenyekiti wa CCM alisema kuwa ameazimia kuwa 2015 upinzani hawatachukua jimbo lolote katika mkoa wa Mwanza. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi wa CCM ambaye alikuwepo ukumbini kama msimamizi mkuu wa uchaguzi huo licha ya kumpongeza Diallo alimtaka aende mbele zaidi kwa kumtaka ashirikiane na wenyeviti wa mikoa mingine kuhakikisha CHADEMA aichukue jimbo lolote kutoka kanda ya ziwa.

MASWALI YA MSINGI.
1. Pascal Patrobass aseme wazi kwanini baada ya kunyimwa ruhusa kazini, je kwanini Dr. Diallo alimpigia simu mkuu wake wa Idara amruhusu aende Dar es Salaam kugombea Uenyekiti wa BAVICHA?
2. Aseme kwanini alitumiwa kwenye uchaguzi wa CCM wa Mkoa kufanya coordination ya wanafunzi wa kike wa shule ya wasichana Bwiru kwenda uwanja wa CCM Kirumba kuhesabu kura?
3. Aseme kuwa nani ambaye alitengeneza pingamizi (draft) dhidi ya wagombea wa CCM mkoa wa Mwanza kwa Joseph Langula Yared na Mabina ambao walikuwa ni tishio kwa Dr. Diallo? Je yalikuwa kwa manufaa ya nani yeye kama ni kweli ni mwanachadema?
4. Akiwa kama mwanasheria wa kanda, aseme kuwa amesha-attend kesi ngapi ya watanzania wa kanda yake ndani na nje ya chama?
5. Je ni kweli amepewa million 12 na Dr. Anthony Diallo?
6. Je ni kweli nauli yake ya ndege kutoka Mwanza kuja Dar es Salaam iliwekewa booking na katibu wa Dr. Anthony Diallo?
7. Aseme kwanini ubia wake na Dr. Anthony Diallo ulianzia pale ambapo alipoanza harakati kutetea haki wanafunzi wa elimu ya juu ya kupiga kura wanafunzi mwaka 2010 hadi Mahakama kuu wakati akiwa SAUTSO? Je kesi ile ilifanikiwa? Kwanini haikufanikiwa? Kwanini punde baada ya kumaliza SAUT akaingizwa Sahara Media Group Limited?
Hitimisho.
Chama kinapaswa kuwa makini sana. Hatuwezi kurisk wakati wapo wagombea wengine ambao hawana hata chembe ya shaka.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments