[wanabidii] UB YAWAASA WATETEZI HAKI ZA BINADAMU

Tuesday, September 09, 2014





UB YAWAASA WATETEZI HAKI ZA BINADAMU 
Na Happiness Katabazi (UB)
CHUO Kikuu Cha Bagamoyo (UB), kimewataka washiriki 10 wa Mafunzo ya utetezi wa Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria toka nchi za Afrika Mashariki( EAC), kuakikisha wanashiriki Mafunzo hayo ili mwisho wa siku waweze kwenda Kwenye nchi zao na Kuwa mabalozi wazuri wa Mafunzo hayo.

Rai hiyo imetolewa juzi jioni  na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB),  anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtaro katika hafla  ya Uzinduzi wa  Mafunzo hayo ya Miezi Sita iliyofanyika Katika Ukumbi wa UB, uliopo Kawe Beach Dar es Salaam.

Dk.Mtaro Alisema Mafunzo hayo yanaendeshwa ndani ya UB  kwa ufadhili  wa Akiba Uhaki Foundation ya nchini Kenya yatasaidia kuwajengea uwezo washiriki Hao ambao wametokea Katika Taasisi za kutetea Haki za binadamu Kuwa na uwelewa mpana Katika eneo Hilo.

' Ieleweke wazi bado wananchi wa EAC Wengi wao hawana uwelewa wa kutosha  kuhusu Haki za Haki za binadamu na ni jinsi gani wanaweza kwenda kuzidai Hao hizo ...hivyo UB  inaamini  kupitia Mafunzo haya ambayo ni ya pili kutolewa na UB yataisidia kuongezeka kwa idadi ya watetezi wa Haki za binadamu Katika nchi za EAC" alisema  Dk.Mtaro.

Aidha Dk.Mtaro alisema bado idadi ya watetezi wa haki za binadamu inaitajika kwani kuna baadhi ya nchi baadhi ya wananchi wa nchi hizo haki zao zinavunjwa wazi wazi na watetezi wa Haki za binadamu wapo wachache hivyo kuna haja ya idadi hiyo ya watetezi kuongezeka ili tatizo hili la uvunjwaji  wa Haki za binadamu likomeshwe.

Kwa Upande wake Mratibu wa Programu ya Mafunzo hayo toka Taasisi ya Akiba Uhaki Foundation ambayo ndiyo inafaa dhili Mafunzo hayo , Kepta Ombati  alisema Taasisi Yao imeamua kushirikiana na UB kutoa Mafunzo hayo  kwa Mara ya pili sasa kwasababu sera na Mitazamo ya UB na Akiba Uhaki zinafanana na kuaidi Kuwa Taasisi hiyo itaendelea kutoa ufedhili kwa UB ili Iweze kuendesha Mafunzo hayo.

Ombati Alisema Mafunzo hayo ya wiki Sita  ambayo ameanza rasmi Jana na kumalizika Februali 22 Mwaka 2015 ,  wanafunzi wanafunzi Hao watapatikana fursa ya kuudhulia Mafunzo   ya darasani  kwa Miezi mitatu na Miezi mitatu itakayosailia wanafunzi Hao wanaenda kufanya utafiti wa Mafunzo hayo kwa njia ya vitendo.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Septemba 9 Mwaka 2014

Sent from my iPad

Share this :

Related Posts

0 Comments