Tamko la Serikali kuhusu uhalali wa bunge maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo September 15, 2014
Hoja ya kusitisha bunge maalum la Katiba imehitimishwa rasmi leo na Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoeleza kuwa bunge lipo kisheria na linaweza kuendelea na kazi zake hadi mwisho wake kisheria.
Waziri wa Katiba na Sheria ameliambia bunge maalum la Katiba usiku huu kuwa wajumbe 500 sawa na asilimia 79 ya wajumbe wote 630 wa bunge hilo wanahudhuria bunge wakati wabunge waliosusia bunge ni 130 pekee sawa na asilimia 21 .
Amesema kundi la wajumbe 201 kutoka makundi mbali mbali ya wawakilishi wa jamii lina wajumbe 189 wanaoshiriki bungeni Kati ya 500 wanaohudhuria bunge hilo.
Amefafanua kuwa wajumbe 348 wanaohudhuria bunge la katiba linaloendelea wanatoka Tanzania Bara Kati yake 125 wanatoka kundi la 201 na kwa wajumbe wanaotoka Zanzibar wapo 152 ambapo Kati yake 64 ni wa kundi la 201 wanahudhuria bunge la Katiba.
Mheshimiwa Migiro amesema bunge linaloendelea hivi sasa lina wawakilishi wanaotoka vyama 18 vya siasa nchini wakati vyama vilivyosusia bunge hilo ni 3 vya Chadema, CUF na NCCR Mageuzi .
Amefafanua kuwa wajumbe waliosusia bunge Maalum la katiba hawafiki theluthi moja ya wajumbe wote hivyo wajumbe walio wengi wanaweza kutumia wingi wao na uhalali wa kisheria na kisiasa kuendelea na majukumu yao hadi Oktoba 4 litakapokoma kisheria.
Amesema wito unaotolewa na baadhi ya viongozi wa kulazimisha kusitisha bunge hilo sio sahihi. Taifa halina mgogoro wa kisiasa. Hakuna sababu ya kuruhusu Watu kujazwa hofu.
" Serikali ipo macho na itasimamia Sheria na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao za kutafuta riziki na mchakato huu uliopo kisheria unaendelea kwa amani" amesema Dr Migiro
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments