[wanabidii] TAMKO LA CHASO LA KUUNGA MKONO KAULI YA MBOWE KUHUSU MAANDAMANO

Wednesday, September 17, 2014

CHADEMA STUDENTS ORGANIZATION (CHASO)
TAARIFA KWA UMMA 
17/09/2014
Jumuhiya ya Wanafunzi wa vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu wa CHADEMA(CHASO) inawatangazia UMMA wa TANZANIA kuwa sisi kama Wasomi wa Vyuo Vikuu na Taasisi zote za Elimu ya Juu -CHASO tumekubaliana kwa Kauli moja KUUNGA MKONO KAULI YA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA Mhe.Freeman A.Mbowe aliyoitoa siku ya Tarehe 14/09/2014 kwenye Mkutano mkuu wa CHADEMA TAIFA,kuwa " endapo KIKWETE,SITA,CCM na SERIKALI isipositisha Matumizi Mabaya ya Fedha za UMMA kwenye BUNGE MAALUM LA KATIBA, kwa kuendelea na Vikao visivyo na TIJA kwa Taifa na kuendelea kutafuna Mabilioni ya Kodi za Watanzania Masikini ,kwa kujifanya wanaandika Katiba ya Watanzania kumbe ni Katiba ya CCM! 
Sisi kama CHADEMA pamoja na UKAWA tutafanya MAANDAMANO,MIGOMO NA MIKUTANO ISIYOISHA MPAKA RAIS KIKWETE ASITISHE BUNGE NA MATUMIZI MABAYA YA MABILIONI YA WALIPA KODI MASIKINI WA NCHI HII''
• CHASO tumekubaliana na tunaunga Mkono Kauli hii ya KISHUJAA ya Kamanda MBOWE.
• Pamoja na hilo CHASO tumepanga kushiriki kikamilifu kwenye Maandamano,Migomo na Mikutano isiyoisha kama ilivyotangazwa Mhe.Mbowe.
• CHASO tumepanga kufanya Maandamano kuanzia kwenye Vyuo Vikuu vyote pamoja Taasisi zote za Elimu ya Juu zilizoko nchi nzima.
• CHASO tumekubaliana kwa kauli moja KUAMBATANA/KUMSINDIKIZA KAMANDA MBOWE Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwenda kuitikia Wito wake wa JESHI la Polisi pale Makao makuu ya Jeshi la Polisi Posta mpya.
Napenda kuwajulisha/Kuwakumbusha wanafunzi wote wa Vyuo vikuu na taasisi zote za Elimu ya juu na UMMA| kwa UJUMLA kuwa Maandamano,Migomo na Mikutano isiyoisha itafanyika kama ilivyopangwa.
Tukutane kama tulivyokubaliana kwa ajili ya Kumsindikiza kamanda MBOWE.

.......................................................................
GANGO P.KIDERA
MRATIBU CHASO KANDA YA DAR ES SALAAM
K.n.y:WARATIBU WA CHASO NCHI NZIMA/KANDA ZOTE

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments