[wanabidii] Scotland yakataa kujitenga na Muungano wa UK.. Watanzania tujifunze na tuimarishe Muungano wetu

Friday, September 19, 2014

Ndugu zangu Watanzania..

Wenzetu wa Scotland wamepiga kura ya maoni na kukataa kujitenga na Muungano wa Uingereza...

Baadhi ya Watanzania wako busy kujenga hoja zisizo na mashiko za kuvunja Muungano wetu wa Tanzania.

Nawashauri Watanzania wote toka bara na visiwani tusidanganyike tukaingia kwenye mtego wa kuvunja Muungano wetu, tuimarishe Muungano kwa kurekebisha kasoro badala ya kujenga hoja za kuvunja Muungano.

Gharama za kuvuna Muungano ni kubwa mno kutokana na mahusiano yaliyojengeka kati ya bara na visiwani, raia wengi wa Tanzania wamezaliwa baada ya Muungano hawajui Tanganyika hivyo tudumishe Muungano wetu ambao ni moja kati ya tunu zetu na unasaidia kudumisha amani, umoja na mshikamano kitaifa.

Mwalimu alituonya tukithubutu kuvunja Muungano kwa hoja nyepesi za wao ni Wazanzibari na sisi ni Watanganyika basi hatutakuwa salama na ni sawa na kula nyama ya mtu, ukizoea hutaacha.

Baada ya kutengana kwa misingi ya ubara na visiwani, tutakuja kutengana kwa misingi ya ukanda, ujimbo, Upemba, Uunguja, kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini, kanda ya kusini n.k...baada ya hapo hatutakuwa salama kama Taifa, kama Watanganyika na kama Wanzanzibari.

Akili za kuambiwa changanya na zako na ufanye maamuzi sahihi.

Idumu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoundwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano ambayo pia inaangalia mambo yote ya Tanzania bara, kama ilivyo Muungano wa Uingereza , eneo la England halina Serikali bali mambo yake yote yanaangaliwa na Serikali ya Muungano ya UK na maeneo mengine ya Wales, Ireland ya Kaskazini na Scotland yana serikali zao ambazo ndizo zinaunda Dola ya Uingereza chini ya Malkia na kiongozi wa Serikali ya Muungano ni Waziri Mkuu.

Niwatakie Watanzania kila la heri katika mchakato wa katiba ambao ndio tunatakiwa wote tuutumie kurekebisha kasoro na keri zote tulizozianisha za Muungano ili tuuimarishe badala ya kuusambaratisha.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Phares Magesa.

Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments