[wanabidii] PROMOTER BRITTS EVENT MATATANI MJINI STUTTGART,UJERUMANI

Sunday, September 07, 2014

 
FUJO Z 30.8.2014 KATIKA SHOW YA DIAMOND HASARA EURO 300,000

PROMOTER BRITTS EVENT MATATANI MJINI STUTTGART,UJERUMANI

Polisi wamesema mpaka kieleweke, M-Nigeria Roho Juu

Stuttgart,Ujerumani,
Anayejiita promota Biritts Event - inayomilikiwa na Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria amejikuta katika mashaka baada ya ripoti ya polisi kuthibitsha jumla ya hasara ya Euro 300,000(Tsh.600 Million) zilizo sababishwa na fujo ya siku ya jumamosi 30 Augost 2014 baada ya msanii wa NASIB ABDUL AKA DIAMOND PLATINUMZ kuchelewa kufika ukumbini mjini Stuttgart,ujerumani.
Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr.Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala wa ukumbi wa
Sindfingen kwa kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya african paty na mkutano sio onyesho la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara ya euro 300,000 ( T-shilingi millioni 600=) ambazo inatakiwa alipe,kwa promota huyo
Awin Williams Akpomiemie hakuwa na bima ya ku-cover au kulinda onyesho hilo na ukumbi lilipofanyika ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki.
taarifa za uhakika polisi imelipeleka swala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt Anwalt)
ya mji wa Stuttgart ili ichukue mkondo wa sheria ambao unamweka roho juu
bwana Awin Williams Akpomiemie - BRITTS EVENTS, Polisi inaendelea 
kumuhoji kwa kujihusika na biashara zingine haramu.

Wakati huo huo tahasisi mbali mbali na jumuiya za wafrika nchini ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa nigeria Awin Williams Akpomiemie
za kuwadanganya washabiki na kulivunjia adhi sifa za bara la Afrika nchini ujerumani ,tahasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa na
m-nigeria huyo Britts Events au Awin Williams Akpomiemie,Pia magazeti mbali mbali ya ujarumani na nchi za kiafrika yameandika BRITTS MAFIA HITS STUTTGART,GERMANY AGAIN !! mojawapo ya gazeti la ghana soma; http://www.modernghana.com/news/567209/1/african-diaspora-is-still-bleeding-diamonds-nightm.html

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments