[wanabidii] Mtandao wa Wanawake na Katiba Wawapongeza Wajumbe wa Bunge la Katiba...!

Friday, September 26, 2014
[caption id="attachment_51307" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-51307" alt="Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0134.jpg" width="640" height="328" /> Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Prof. Ruth Meena (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi na wajumbe wengine wa mtandao wa wanawake na Katiba.[/caption]

[caption id="attachment_51306" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-51306" alt="Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0139.jpg" width="640" height="310" /> Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari.[/caption]

[caption id="attachment_51311" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-51311" alt="Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_01441.jpg" width="640" height="432" /> Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.[/caption]

[caption id="attachment_51304" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-51304" alt="Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_01461.jpg" width="640" height="367" /> Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.[/caption]

[caption id="attachment_51308" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-51308" alt="Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo." src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0130.jpg" width="640" height="332" /> Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.[/captio[caption id="attachment_51313" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_01911.jpg" alt="Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Usu Mallya (katikati) akizungumza katika mkutano huo na wanahabari." width="640" height="394" class="size-full wp-image-51313" /> Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Usu Mallya (katikati) akizungumza katika mkutano huo na wanahabari.[/caption][caption id="attachment_51314" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0173.jpg" alt="Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo." width="640" height="369" class="size-full wp-image-51314" /> Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.[/caption][caption id="attachment_51312" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/IMG_0171.jpg" alt="Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo." width="640" height="357" class="size-full wp-image-51312" /> Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.[/caption]n]

<strong>MTANDAO</strong> wa Wanawake na Katiba Tanzania umewapongeza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na hasa wajumbe waliokuwa mstari wa mbele kupigania masuala mbalimbali yaliyokuwa yanapendekezwa na mtandao huo juu ya uwepo wa Katiba inayopendekezwa yenye mtazamo wa kijinsia.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma tayari kwa zoezi la kuanza kupigiwa kura kifungu kwa kifungu na wajumbe wa bunge hilo.

Prof. Meena alisema Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania haunabudi kuwapongeza wajumbe wote wa bunge maalum na hasa wale waliowaunga mkono kupaza sauti juu ya madai ambayo waliwasilisha kupitia mtandao wao na njia nyingine mbalimbali kushinikiza katiba inayopendekezwa kuwa na mlengo wa kijinsia ili kutoa usawa wa kijinsia.

Alisema Rasimu ya Katiba inayopendekeza imeonesha mwelekeo wa kutoa usawa wa kijinsia jambo ambalo mtandao huo unaamini ni mafanikio makubwa kwao na kwa jamii inayojali usawa wa kijinsia. Aliongeza kuwa yapo mambo kadhaa ambayo walipendekezwa yatajwe kwenye katiba kama umiliki wa ardhi kumtambua mwanamke na kutajwa kwa umri wa mtoto jambo ambalo wanaamini litapunguza kilio cha ndoa za utoto suala ambalo wanaharakati wa masuala ya kijinsia wamekuwa wakilipigia kelele siku zote.

"...Tunapenda kutoa pongezi kwa wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa moyo waliouonesha kujali masuala ya kijinsia kwa kiasi chake...tunaunga mkono rasimu ya Katiba inayopendekezwa kwa kuamini ni mwanzo mzuri wa kuonesha usawa wa kijinsia...," alisema Prof. Meena akizungumza na wanahabari.

Kwa upande wake Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Usu Mallya akizungumza alisema licha ya mafanikio yao kwa mtandao wao wamehoji baadhi ya mapendekezo ambayo yamekataliwa na wajumbe hao ilhali yanamuelekeo mzuri juu ya uwajibikaji wa wanasiasa kwa wapigakura wao.

Alisema wameshangazwa na kitendo cha wajumbe wa bunge la katiba kuruhusu kipengele ambacho kimeweka utaratibu kuwa Rais wa nchi anaweza kushtakiwa ilhali wamepinga kipengele za kutoa fursa kwa wapiga kura kumuwajibisha mbunge wao baada ya kumchagua pale wanapoona ameshindwa kuwawakilisha kama walivyokubaliana.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

&nbsp;

______________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments