[wanabidii] MAHAKAMA YA KADHI YAMESABABISHA KATIBA MPYA ISIPATIKANE

Sunday, September 14, 2014
Wiki iliyopita CCM walikubaliana, kwa kauli moja, kuipotezea Mahakama ya Kadhi na wakaafikiana kwamba wasiongelee suala hilo tena bungeni au mahali popote pale. Lakini kutokana na jeuri ya Samweli 6 tumeona suala hilo likijadiliwa bungeni, tena kwa hisia kali sana. Ni dhahiri kwamba suala hili ndilo litakuwa msumsri wa mwisho kwenye katiba hii iliyotekwa na CCM. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo:
 
1.      Waislamu tayari wamejiwekea matumaini makubwa kwamba suala hili litaingizwa kwenye katiba kama ambavyo wamekuwa wakiomba kwa muda mrefu. Sasa ikiwa itakuwa kinyume chake, ni vigumu sana wabunge waislamu waliomo Bunge la Katiba kukubali kupitisha katiba iliyopendekezwa ambayo haitakuwa na kipengele cha Mahakama ya Kadhi. Au ikiwa CCM watawashawishi waislamu waliomo bungeni, kwa namna yoyote ile, hadi wakakubali kuipigia kura katiba niliyopendekezwa, mashehe wote waliomo bungeni watafute dini zingine za kuabudu na wasirejee hapa uraiani. Vinginevyo patachimbika! Kwa jinsi waislamu walivyo hodari kutetea maslahi yao, hawatakuwa tayari kusalitiwa na mashehe wachache kwa maslahi yao binafsi.
 
Aidha waislamu waliopo uraiani hawatakubali kuipigia kura katiba iliyopendekezwa ambayo haitakuwa na kifungu kinachoongelea kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi. Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba katiba hii haitapita. Kumbuka kwama idadi ya waislamu ni kubwa kuliko ya wakristo (kwa mujibu wa uatafiti wa TBC). Kwa hiyo kama wataamua kupiga kura za HAPANA kwa katiba iliyopendekezwa, hakutakuwa na katiba mpya bali itabidi turejee katika matumizi ya katiba ya mwaka 1977, huku tukisubiri Serikali ya UKAWA waje watupe katiba mpya mwaka 2016.
 
2.      Na ikiwa katiba iliyopendekezwa, itapendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, wakristo nao hawatakubali katiba hii ipite. Na mkwamo huu utakwamia bungeni hata kabla ya kufika kwa wananchi. Kumbuka kwamba Baraza la Katiba (BMK) lina wakristo wengi kuliko waislamu. So, ikiwa wakiamua kupiga kura za kuikataa katiba yenye Mahakama ya Kadhi, akidi haiwezi kutimia. Hivyo suala la kukataliwa kwa Katiba hiyo litamalizikia kule kule bungeni. Ijapokuwa kuna wachungaji na maaskofu mapandikizi wa CCM mnaowaona mle bungeni, linapokuja suala lolote la kidini, msimamo wao huwa haubadiliki. Hawawezi kukubali kujiharibikia kazi ya kudumu (uchungaji/uaskofu) kwa sababu ya kutetea kazi ya muda (ujumbe wa bunge la katiba) waliyopewa na CCM. Lazima watasimama upande wa kazi ya kanisa kuliko kazi ya CCM.
 
Pamoja na kwamba wanaweza kuahidiwa mambo makubwa na CCM hadi wakajisahau na kuunga mkono katiba ya CCM, pindi wakirejea huku uraiani hakutakalika! Itapaswa wakatafute dini zingine za kuabudu kwa kuwa watakuwa wamewasiliti wakristo waliowatuma bungeni kuwatetea lakini wakatekwa na CCM na kuasahau walichotumwa. Aidha, ikiwa itatokea wameshwishiwa na kukubali kuiptisha katiba hiyo, wakristo waliopo hapa uraiani wataikakataa katiba iliyopendekezwa na kwa maana hiyo hakutakuwa na katiba mpya. Hivyo katiba ya mwaka 1977 itaendelea kutumika hadi Serikali ya UKAWA itakapotupa Katiba ya Wananchi mwaka 2016.
 
HITIMISHO
Kwa hiyo ndugu zangu, mtaona kwamba suala hili la Mahakama ya Kadhi ndio litakuwa msumari wa mwisho kwenye katiba hii ya CCM, kwa maana kwamba Mahakama hiyo, ama iingizwe au isiingizwe kwenye katiba mpya au la, bado itakuwa ni kikwazo kwa upatikanaji wa katiba mpya, kama nilivyonyambulisha hapo juu. Simlazimishi mtu kukubali au kukataa maoni haya lakini UKWELI utabakia kuwa hivyo – kwamba suala la Mahakama ya Kadhi tayari limeishavuruga upatikanaji wa katiba ya CCM. Huu ni ushindi kwa wananchi ambao katiba yao ilikuwa imetekwa na CCM. Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Saweli 6 kwa kukiuka makatazo ya CCM, ambao walikataza suala hili lisizungumzwe bungeni, lakini kwa kutumia jeuri yake binafsi, akaamua kuwaruhusu mashehe waongelee suala hili na hivyo kuibua muamko mpya kwa wabunge na wananchi kuikataa katiba ya CCM.
 
Nawasilisha.

Share this :

Related Posts

0 Comments