[wanabidii] IGOMBEI URAIS 2015 ASEMA MHE JUMA NKAMIA

Tuesday, September 16, 2014
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni , Mbunge wa Kondoa Kusini amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya urais 2015 kama viongozi wengine wanavyotangaza nia huku akidai kuwa kazi yake kubwa nikuhakikisha wananchi katika jimbo lake wanapata maendeleo kupitia nafasi yake ya  ubunge

Waziri Nkamia aliyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara fupi katika kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,ambapo alisema kuwa hajawa na ndoto ya kuwa Rais 2015

Alisema kuwa kiongozi anayestahili kuwa rais ni lazima awe na uwezo wa kuongoza na anayekubalika na watanzania na vigezo isiwe umri wa mtu

"Pamoja na umri nilionao 42 sina mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015 na umri usiwe kigezo cha kugombea uwezo wa kiongozi ni muhimu sana"alisema Nkamia

Pia Waziri huyo aliipongeza kituo hicho cha redio kwa kazi nzuri ya kuburudisha na kuelimisha jamii kupitianvipindi vyake mbalimbali huku akiwataka kuandaa vipindi ambavyo vitawashirikisha wachezaji wazamani hali itakayosaidia kukuza na kuibua changamoto katika michezo

http://jamiiblog.co.tz/2014/09/15/sigombei-urais-2015-asema-nkamia/

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments