[wanabidii] Gross Mistreatment by BBC Kiswahili Jana Usiku

Friday, September 26, 2014


Naamini BBC Kiswahili wangeweza kufanya kitu bora zaidi kwenye habari yao ya kwanza jana,lakini waliamua kufanya hivi tu:
1.IPhone 6 na Plus yake zinapinda-kutokana na ushahidi toka wa watumiaji.
2.IPhone 6 na Plus zinatengenezwa na kampuni ya Apple ya Marekani.
3.Mahojiano na mtumiaji wa Apple anayeishi Dar es Salaam. Ndani ya mahojiano hayo, binafsi nilitarajia kusikia zaidi, pengine hata aliyekuwa anamhoji mtumiaji wa Dar angetaka kusikia zaidi, lakini bila shaka mtumiaji asingeweza kujibu maswali yote. Kwa mfano mtumiaji pamoja na maswali megine ya kitumiaji aliulizwa: Iwapo mauzo yataathirika? Iwapo kutokuwepo kwa Steve Job kumeathri Apple; Kama ku bend ni tatizo. Mtumiaji alisema kila kitu si tatizo.

Naamini BBC ingeweza kupata stori iliyojaa zaidi ya hiyo. Nilibaki najiuliza hivi Apple hawana hata commissioned vendor, company representative hapo jijini London? Hawana customer/ama media relations personnel. Kwa kampuni iliyo kwenye ushindani na ikapata mkasa kama huu ndani ya wiki moja tangu kutoa kifaa kipya, naamini wasemaje wake wangekuwa wanasubiri ama wanatafuta fursa za kuongea na jamii, ili waseme iwapo nini ni tatizo na je wateja wao waliopata shida na kifaa hicho wangepata hasara ya fedha ama wangepewa kifaa kingine/ama je ni tatizo la kiufundi ama nini kimetokea. Bila shaka wao ndio wangeweza kujibu baadhi ya maswali aliyoulizwa mtumiaji wa Dar es Salaam.

Lakini hata Dar kuna dula la Iphone. Pengine hata angeweza kuulizwa mtumiaji wa Iphone ametua miaka mingapi ili BBC iwaweke watazamaji wake kwenye ukurasa mmoja nao kuamini maoni ya msikilizaji mwenzao ambaye ameitwa kutoa, 'expert' opinion ya namna fulani. Je, alikuwa anaongelea iphone 6?

Ungeniuliza kutoa alama kwa ile habari ya kwanza ya jana ya BBC Kiswahili ningetoa 25 ya mia moja, kwa kuwa wemefanya robo tu ya kazi.

Binafsi naamini kuwa kutoka BBC, tunastahili kupata ubora zaidi ya huo. Pia najua mnaweza.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments