[wanabidii] FAHAMU HAKI NA WAJIBU WA MPIGA KURA KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA

Tuesday, September 16, 2014
Mchakato wa uchuguzi wa viongozi kwa njia ya kidemokrasia ,hufanywa kwanjia ya kupiga kura .huu ndio wakati ambao kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 na zaidi hushiliki kuchagua viongozi wa kushika madalaka ya dola na uakilishi kwa kipindi cha miaka 5 kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Ili mtu aweze kupiga kura sheria inaelekeza kwamba,ni lazima awe amejiandikisha na kupewa kitambulisho kinacho muwezesha kutambulika kwamba ni mpiga kura alali wa kituo husika.
Hivyo,ilikuepuka kutenda kosa au ukiukwaji mwingine wa sheria katika zoezi la uandikishaji ni muhimu kumbuka kwamba :
• Nikosa kujiandikisha mara mbili
• Ni kosa kutoa taarifa za uongo kwa fisa muandikishaji
• Nikosa kuuza au kununua kitambulisho cha kupiga kura.
• Nikosa kufanya vurugu katika kituo cha kuandikisha wapiga kura
• Nikosa kufanya kampeni katika kituo cha kuandikisha wapiga kura
UTEUZI WA WAGOMBEA NA MHIMILI WA AMANI NA USALAMA WA JAMII
Uteuzi wa wagombea kupitia vyama vya siasa vilivyosajiliwa ,hufanywa baada ya wagombea kuchukuwa,kujaza na kurejesha fomu za kuomba vyama vyao kuwapendekeza wagombee kwa tiketi ya vyama vyao.Hatua hii ni muhimu kwa sababu vyama uawashindanisha wanachama wao,ili kumpata mgombea aliye bora .
Wakati wa mcahakato huu vyama vya siasa kwa kutumia kanuni za katiba zao,vina wajibu wa kuakikisha wagombea au mawakala wao hawakiuki sheria za nchi .Pia ndio wakati wa kumthamini mgombea ,kama anaweza kuleta maendeleo yanayozingatia mhimili wa amani ,usalama na utulivu kama mtaji wa maendeleo ya jamii anayoomba kupewa fursa ya kuingoza.
HARAKATI ZA KAMPENI NA USHAWISHI
K ampeni ni ushawishi wa nguvu ya hoja na sera wenye lengo la kuomba kuchaguliwa na wapiga kura.Kwa sababu kula pekee ndiyo inayotoa ridhaa kwa mgombea kushika madalaka ya dola au uwakilishaji katika mamlaka za maamuzi.
Kampeni na ushawishi na humwezesha mpiga kura kuwafahamu wagombea ,vyama vyao na sera zao.
Sheria inatoa uhuru wa kampeni kufanywa nyumba kwa nyumba,kujitangaza kupitia vyombo vya habari,kubandika matangazo au mabango,mikutano ya adhala n.k
Katika hatua hii ni muhimu kila mwanajamii hakafahamu na kuepuka makosan yafuatayo:-
• Kufanya kampeni kabla ua baada ya muda ulioruhusiwa
• Kutumia lugha ya matusi,kashfa au uongo katika kampeni na ushawishi
• Kueneza uongo dhidi ya mgombea wa chama chochote
• Kuwatisha,kuwabughudhi au kuwazuia wapiga kura
• Kufanya fujo au vurugu.
• Kutoa au kupokea rushwa n.k 
• Kumbuka mtu akitenda kosa, sheria itachukua mkondo wake.
-Kila mgombea anao wajibu wa kuwaelimisha wafuasi wake umuhimu wa amani,usalma na utulivu kabla na baad ya uchaguzi.
HARAKATI ZA KAMPENI NA USHAWISHI
Pia ni wajibu wetu kutambua kwamba :-
-Nikosa kuondoa,kuchana au kubandua matangazo ya wagombea .
-Nikosa kuandika maneno mengine kwenye matangazo hayo.
-Nikosa kubandika matangazo katika maeneo au sehemu zisizo ruhusiwa au juu ya tangazo la mgombea mwingine(kuliziba).
WAJIBU NA UMUHIMU WA POLISI KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI
Polisi ni chombo cha umma,akitumikii chama chochote cha siasa bali ni chombo kinacho wajibika kutenda kwa haki na usawa bila upendeleo katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Pamoja na wajibu wa kulinda amani na usalama wa raia wote,katika kipindi cha uchaguzi utekelezaji wa majukumu unaweka mkazo katika mambo yafuatayo:-
Kuhakikisha mikutano ya kampeni inafnyika na kumalizika salama 
Kuahakikisha kwamba zoezi la upigaji kura linaenda sawa,bila vikwazo au bughudha.
Kuhakikisha kwamba vifaa vya kupiga kura viko salama yaani aviibiwi,wala kughushiwa na watu wenye nia mbaya .
Kuhakikisha mchakato wa kupiga kura,kuhesabiwa na kutangazwa matokeo unakuwa huru na haki.
Kuhakikisha amani,usalama na utulivu vinadumu kabla na baada ya matokeo kutangazwa.
UWEPO WA POLISI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI,NI ILI KUISHILIKISHA JAMII KUDUMISHA AMANI NA USALAMA. 
HAKI NA WAJIBU WA MPIGA KURA
Kupiga kura ni haki ya msingi ya kila Mtanzania aliyetimiza umri unaokubalika kisheria.Lakini haki iyo inaambatana na wajibu mbalimbali,ikiwemo umuhimu wa kujielimisha kuhusu sheria na utaratibu zinazo husu mchakato mzima wa uchaguzi.
Kwasababu endapo mpiga kura atavunja sheria atashtakiwa.Kisingizio cha kutojua sheria iliyovunjwa,sio sababu ya kutokamatwa na kushtakiwa.Hivyo kutii sheria na taratibu za uchaguzi ni wajibu.
SIKU YA UCHAGUZI
Siku ya uchaguzi inapowadia,kila mtu aliyejiandikisha ,anawajibika kwenda na kitambulisho chake cha mpiga kura katika kituo alicho jiaandikisha.
Kituoni atawakuta wasimamizi wa uchaguzi watakao mwelekeza utalitibu wenye lengo la kurahisisha zoezi hilo.Huo ndio wakati wa kutumia haki ya kidemokrasia ya kumchagua kiongozi unayemtaka.Lakini haki hii inaambatana nawajibu,ambao unatutaka kuepuka mabo yafuatayo:-
Kutumia uvumi,maneno ya uongo,hisia au visingizio vyenye lengo la kuzuia wengine kwenda kupiga kura
Ni kosa kufanya kampeni katika kituo cha kupiga kura 
Ni kosa kupiga kura kwa kutumia jina na kitambulisho cha mtu mwingine,aliyefaliki au kutumia jina la uongo
Ni kosa kupiga kura zaidi ya mara moja.
Ni kosa kuvaa nguo zenye picha za wagombea,maneno au nembo ya ama rangi za chama cha siasa.
Ni kosa kufanya fujo kwenyekituo cha kupiga au mahara popote.
Ni kosa kuhamasisha watu kukusanyika na kufanya vurugu.
Baada ya kupiga kura ni muhimu kuondoka kituoni,ili kuepuka uwezakano wa kusababisha mikusanyiko inayoweza kutafsiliwa kuwa ni haramu.
KUHESABIWA NA KUTANGAZWA MATOKEO YA UCHAGUZI
Mara baada ya kura kupigwa na zoezi hilo kufungwa rasmi, hatua inayofuata ni kuzichambua na kuzihesabu kura ili kupata matokeo.Kwa kawaida zoezi hili ueendeshwa kwa uwazi mbere ya maafisa wenye dhamana ya usimamizi wa uchaguzi,mawakala wa vyama na vyombo vya ulinzi na usalama ususani polisi.Jamii aipaswi kuingiwa shaka,bali tunapaswa kuwa na subira ili kutuo fursa kwa wahusika kukamilisha mchakato huo.Hivyo ni vema kila mwanajamii akatambua mbio za siasa za kugombea uongozi wa umma,huishia kwenye sanduku la kura.Huu ni ukweri kwa sababu kwenye ushindani lazima apatikane mshindi ndi sababu baada ya kutangazwa chaguo la wengi,sote tunawajibika kumkubali,kumuheshimu,kumtambua na kushilikiana naye ili aweze kutimiza wajibu wake kama kiongozi wa watu wote.
KUMBUKA,Kipaumbere ni usalama na kabla na baada ya uchaguzi.
UVUNJAJI WA SHERIA WAKATI WA UCHAGUZI
Vitendo vyovyote vya uvunjwaji wa sheria kabla na baada ya uchaguzi,ni uhalifu.Sheria haina udhuru,inachukua mkondo wake mara moja ukiukwaji umefanyika.Harakati za mchakato wa uchaguzi ,haipaswi kuchukuliwa katika mtazamo mbaya wa kahalalisha vitendo vya kihuni au vurugu.Bali ni nyenzo inayotupa fursa ya kupata viongozi watakao tuwezesha kupiga hatua kueelekea katika maendeleo na ustawi wa kijamii katika Nyanja zote.
Tuelimishane ili kuepuka makosa au uharifu kabla na baada ya uchaguzi.Huo ndio msingi wa ulinzi shilikishi katika mchakato mzima wa uchaguzi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments