Ajali iliyotokea hivi leo katika barabara ya Mwanza Musoma na kuua watu 26 na kujeruhi 70, imetia simanzi na kukumbusha machungu tunayoyapata kutokana na uharibifu mwingi utokanao na ajali barabarani.
Tunapoteza ndugu zetu. Magari yanaharibika na kugarimu fedha nyingi kuyatengeneza na barabara pia kuharibika na hasara nyingi ambazo kila mtu anaona.
Mara nyingi sababu kubwa ni uzembe wa madereva wetu. Hata pale ambapo tunasema barabara ni mbovu lakini ijulikane barabara hiyo mbovu ikipitwa kwa uangalifu ajali haziwezi kutokea.
Sasa kama chanzo ni madereva wetu tujiulize madereva wetu wanapatikanaje?
Napenda kuanzia mbali kidogo.
Mtu akiuliza tunapataje waganga na madaktari au manesi mimi najua kuwa kuna sifa za kuingia chuo cha waganga au manesi. Mtu asipozitimiza hawezi kusomea fani hiyo. Kuna mtaala umeandaliwa na walimu waliobobea wanaandaliwa kuwaandaa wataalam hawa. Kileleni mwa masomo yao utakuta wataalamu kutoka vyuo na hospitali mbalimbali wanaelekea kwenye vyuo vya wataalamu hawa kuwatahini. Najua kabisa kuwa walimu husika hawaruhusiwi kuwataini wanafunzi waliowafundisha ila wanatoka nje ya chuo husika.
Naelewa kuwa wote tunajua hekaheka zinazokuwepo wanafunzi wa darasa la saba wanapokuwa wakifanya mtihani. Si idara ya elimu peke yake, Usalama wa taifa, Polisi nakadhalika. Wote hukusanyika kuhakikisha mitihani inafanyika salama. Nikomee hapo lakini tunayo mifumo ya kuwapata walimu, askari nakadhalika.
Madereva wetu wanapatikanaje? Kichekeso. Madereva walio wengi walikuwa utingo wa mabasi au malori. Kuna wakati unakuta mtu ana liseni ya udereva kabla hajajua kuendesha gari. Kuna wakati unaona mtu anafika chuo cha madereva na kulipa kila kitu lakini bila kuhuzulia masomo anapata vyeti.
Umefika wakati sasa wizara husika kuweka utaratibu. Utaratibu wa kuwapata madereva ikiwa ni pamoja na mitaala, sifa za kuingia vyuoni na namna ya kuwatahini wahitimu. Tumeona nchi za wenzetu wana mifumo kama hii. Kuna passenger drivers, heavy duty drivers. Track driving schools nakadhalika. Tukiwaandaa wataalamu wetu hawa na kuhakikisha wanapata maadili chuoni tutapunguza ajali zinazoonekana sasa kwa kiwango kikubwa.
Nakumbuka pia kujifunza sheria za barabarani kutokana na madaftari niliyokuwa nayatumia shuleni enzi hizo nchini Uganda. Tuna madaftari nyingi zinatangaza biashara mbali mbali. Tunaweza kuweka taratibu kama hizi ukakuta watoto wetu wanaelewa sheria za barabarani hata wakingali shuleni. Pasipokuwa na mikakati maalum kama hiyo tutaendelea kuumia.
Tunasemaje wengine?
Elisa Muhingo
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments