[wanabidii] Vyama vya Siasa kukutana na Rais Kikwete kuhusu Katiba Mpya

Wednesday, August 27, 2014
Vyama vyote vya siasa nchini vinatarajiwa kukutana na Rais Jakaya Kikwete kabla ya mwisho wa wiki hii, kujadiliana na kushauriana juu ya maendeleo ya mchakato wa Katiba mpya. 

Vyama hivyo vya siasa vitakutana na Rais kwa mwavuli wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na vitakutana siku yoyote kuanzia leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana juu ya kikao hicho, Mwenyekiti wa TCD ambaye pia ni Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo alisema baada ya kukutana Agosti 23 mwaka huu, viongozi wa vyama hivyo walikubaliana kukutana na Rais Kikwete, ndipo walipomuandikia barua ya kumuomba akutane nao na Rais akawajibu kuwa atakutana nao kabla ya mwisho wa wiki hii.

Vyama hivyo vya siasa ni pamoja na vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambavyo ni CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi ambavyo viongozi wake wamethibitisha kushiriki. Vingine ni CCM, TLP, UDP na UPDP inayowakilisha vyama visivyokuwa na wabunge.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments