jana nilipata nafasi ndogo kusikiliza mjadala bungeni.
Moja kati ya mambo niliyoyasikia ni kuongeza vifungu vinavyohusu ardhi.
Kwa kumbukumbu zangu Tume ya Katiba iliviacha vifungu hivyo ili viingizwe kwenye katiba za nchi washirika.
Kuvijadili katika hatua hii maana yake tayari uamuzi wa muundo wa serikali ni wa serikali mbili.
Kama hilo halijatatuliwa basi kusingekuwa na maana kuwataka UKAWA kuja bungeni sasa zaidi ya kuja kujadili muundo wa muungano.
Kwa sababu hiyo hakukuwa na maana ya kuwaomba ukawa kurudi bungeni wakati hawakuwa na cha kujadili. Wao wanaweza kuja bungeni kujadili rasimu iliyowakilishwa na tume wakati bunge sasa linatengeneza katiba mpya nje ya ile licha ya kujiambia (hawatwambii sisi) kuwa wanajadili rasimu hiyo. Nafikiri inafaa ku-replay maneno ya Pro. Kabudi.
0 Comments