[wanabidii] TAARIFA KUHUSU HAKI ZA MTOTO NA MAREKEBISHO YA TABIA

Monday, August 18, 2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

TAARIFA KUHUSU HAKI ZA MTOTO NA MAREKEBISHO YA TABIA

Idara ya Ustawi wa Jamii ina jukumu la kusaidia ,kutatua matatizo ya wananchi kwa kutoa ,kusimamia na kuratibu huduma za ustawi wa jamii kwa kujumuisha huduma za familia, watoto na malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto, huduma kwa wazee na watu wenye ulemavu pamoja na huduma za marekebisho,ujenzi wa tabia na haki za mtoto kisheria ambazo zinatolewa kwa misingi ya ushirikishwaji wa jamii. Kwasasa huduma hizi zinatolewa chini ya vitengo vinne ambavyo ni:-
Marekebisho Tabia na haki za mtoto kisheria
Ustawi na familia, watoto na malezi, makuzi na maendeleo yaawali ya watoto
Huduma kwa watu wenye ulemavu na 
Maendeleo ya watumishi wa kada ya maafisa ustawi wa jamii
Leo ningependa kuzungumzia kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia kina jukumu la kuratibu huduma za mpango wa majaribio wa marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria katika jamii, huduma kwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani, huduma katika mahakama za watoto na waathirika wa pombe na dawa za kulevya. 
Watoto waliokinzana na sheria wanaotunzwa katika mahabusi tano za watoto zilizopo katika mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Dar es Salaam na katika Shule ya Maadilisho ya Irambo – Mbeya,

Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto, watoto wanaokinzana na sheria na ambao hawajapata dhamana kutoka kwa mahakama wanapasa wapelekwe katika mahabusu za watoto na pale ambapo mahakama imejiridhisha kwa ushahidi na kumtia mtoto husika hatiani basi kwa mujibu wa sheria hii hakimu/jaji anapaswa kuamuru mtoto huyu kupelekwa katika shule ya maadilisho. 
Huduma za mahabusu za watoto
Mahabusu za watoto ni mahususi kwa ajili ya kuwahifadhi, kuwatunza na kuwarekebisha watoto walinatuhumiwa kufanya makosa mbalimbali ya jinai na ambao wamekosa dhamana. Huduma zinazotolewa ni pamoja na ushauri na unasihi, bustani na ufugaji, elimu ya msingi na ufundi stadi, huduma za kiroho na michezo.
Huduma ya maadilisho kwa watoto waliotiwa hatiani na kupelekwa katika shule ya maadilisho 
Huduma hii ni kwa ajili ya marekebisho ya tabia za watoto waliotiwa hatiaani kwa makosa mbalimbali ya jinai na mahakama. Huduma zinazotolewa ni pamoja na ushauri na unasihi, kilimo na na ufugaji, elimu ya msingi na ufundi stadi, huduma za kiroho na michezo kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu. Aidha kumekuwapo na kuboreka kwa huduma ya marekebisho ya tabia kwa watoto waadiliwa kwani wengi wao wamekuwa wakifaulu mtihani wa elimu ya msingi. Jedwali lifuatalo linaonesha:

Jedwali: Mwenendo wa ufaulu wa waadiliwa katika mtihani wa darasa la saba katika Shule ya Maadilisho Irambo 2009-2013.

Mwaka Darasa VII Waadiliwa Waadiliwa waliofaulu Asilimia 
2009 20 8 7 87.5%
2010 20 15 6 40%
2011 10 7 3 42%
2012 10 6 6 100%
2013 6 5 83.3%

Mpango wa kijamii wa marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria
Serikali imeanzisha mpango wa kuchepusha watoto walio katika mkinzano na Sheria na walio katika hatari ya kukinzana na Sheria katika jamii mashauri yao kutokupitia katika mfumo rasmi wa kisheria. Mpango huu wa majaribio ya marekebisho ya tabia unatekelezwa katika halmashauri ya manispaa ya Temeke na hadi sasa jumla ya watoto 132 wamenufaika na mpango huu. Vigezo vya kuwapokea/ ingiza watoto katika mpango. huu ni pamoja na Umri ( 10 – 17), kukiri kosa, kosa lazima liwe dogo,ridhaa ya wazazi na mtoto husika, pia awe mkazi wa eneo hilo. 
Mafanikio 
• Kukamilika kwa Kanuni za Mahabusi za watoto,Makao ya watoto na Shule ya Maadilisho
• Kukamilika kwa miongozo ya utoaji wa huduma katika Mahabusi za Watoto na Shule ya Maadilisho ; 
• Kukamilika kwa Mwongozo wa wa kijamii(CRP) wa Marekebisho ya Tabia kwa Watoto waliokatika Mkinzano na Sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria
• Kuwajengea uwezo watumishi wote wa Mahabusi za watoto na shule ya maadilisho juu ya miongozo mbalimbali iliyotolewa ya kuboresha huduma katika taasisi hizo 
• Kuanzishwa kwa program/ mradi wa (majaribio) wa huduma kwa watoto wanaofanya kazi na kuishi mtaani katika mkoa wa Dar es salaam
• Kuanzishwa kwa muendelezo wa (CRP) katika mkoa wa mbeya.
• Kukamilika mahabusu ya watoto ya Mtwara kwa asilimia 95
• Kukamilika kwa bweni la wasichana Irambo kwa asilimia 98

Changamoto
Changamoto kubwa ni upungufu wa maafisa ustawi wa jamii katika halmashauri wanaotoahuduma kwa watoto walio katika mikinzano na sheria.
Wizara kupitia idara ya ustawi wa jamii imekuwa ikishirikiana pamoja na wadau mbalimbali kama vile polisi, Mahakama, magereza, tume ya haki za binadamu na utawala bora pamoja na mashirika mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa katika kufanikisha na kutekeleza majukumu yake.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments